July 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Bodaboda: Tunatumiwa na wanasiasa

Spread the love

UONGOZI wa waendesha bodaboda jijini Dar es Salaam umekiri kutumiwa na wanasiasa katika harakati zao za kisiasa. Anaandika Sarafina Lidwino … (endelea).

Akijibu swali la mwandishi wa Mwanahalisionline aliyetaka kujua kuhusu taarifa za kutumiwa na wanasiasa, Mwenyekiti wa Madereva wa Bodaboda katika Wilaya ya Ilala, Saidi Kagomba amesema, wanafanya hivyo kwa kuwa ni sehemu ya biashara.

Amefafanua kuwa, kazi hiyo hufanywa baada ya kuingia makubaliano maalumu na wanaiasa ama mwakilshi wa chama.

“Ndio tunatumiwa sana lakini kibiashara na hata kama kunamwendesha bodaboda ana mapenzi na mgombea fulani anahaki ya kuhudhuria kwani kila mtu ana chama chake,” anasema.

Amesema, waendesha bodaboda ni wafanyabiashara hivyo wanahaki ya kufanya kazi yoyote ili mradi walipwe kulingana na kazi.

“Kuna vituo vingi vya bodaboda hivyo hutokea tenda za kuwabeba watu au kwenda katika maandamano hivyo sisi hatuwezi kuzikataa tenda hizo. Tunaandikishana kwa ruti tutakazopiga na tunapewa malipo yetu,” amesema.

Aidha, viongozi hao wamesema wapo tayari kushirikiana na kiongozi yoyote ambaye atawajali na kutatua matatizo yao.

Hata hivyo, uongozi huo umepinga vikali kauli iliyotolewa na aliyejiita kiongozi wa bodaboda kwamba hawana matatizo.

Jana wakati wa ufunguzi wa kampeni za mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli kwenye Uwanja wa Jangwani jijini Dar es Salaam, Mapinduzi Mpema alipanda jukwaani kwenye mkutano huo na kudai “nimetumwa na bodaboda nisema kwamba, hatuna matatizo.”

Kagomba amesema, hawajamtuma Mpema kuwasemea kwenye mkutano huo na kwamba, amenunuliwa.

“Tunajua amenunuliwa afanye hivyo, huyu ni dereva kama madereva wengine wa bodaboda, hatujamtuma na wala si mwakilishi wetu.

Angekuwa kiongozi kama sisi lazima angejua matatizo yetu,” amesema Kagomba.

Kwenye mkutano wa CCM Mpema amenukuliwa akisema, anaishukuru Serikali ya CCM kwa kuwaletea ajira vijana wakiwemo bodaboda na kwamba hawana matatizo yoyote. Wanafanya kazi zao vizuri.

Kagomba amesema, walishangazwa na kitendo alichofanya Mpema kwani viongozi hawakuwa na taarifa naye juu ya utoaji wa taarifa ya umoja huo na kuwa, aliyaficha mengi yanayowasibu na kuisafisha CCM.

Akielezea matatizo yanayowasibu bodaboda kwa muda mrefu amesema, wamekuwa wakikamatwa mara kwa mara bila sababu, wanatozwa pesa nyingi pamoja na kupangiwa njia (ruti) katika kazi zao ikiwemo kuzuiwa kwenda katikati ya jiji.

“Mara baada ya mkutano ule kuisha jana, nilipigiwa simu nyingi sana kutoka mikoani. Madereva wengi walisikitishwa na kauli zake na hivyo kutuomba viongozi tutengue kauli zake na serikali itambue kuwa tunamatatizo mengi.

“Tunaomba serikali iwe makini sana na watu kama hao kwani wanaweza kusababisha uvunjifu wa amani,” amesema Kagomba.

error: Content is protected !!