May 29, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Bocco: Tunakwenda kupambana

John Bocco, Nahodha wa Simba

Spread the love

 

Nahodha wa klabu ya Simba John Bocco anaamini kuelekea mchezo wa marudiano dhidi ya Kaizer Chiefs watahakikisha wanapambana ili kuondoka na matokeo mara baada ya kukubali kichapo cha mabao 4-0 kwenye mchezo wa kwanza uliopigwa Afrika Kusini. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Mchezo huo wa marudiano utapigwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam majira ya saa 10 jioni.

Bocco ameyaongea hayo wakati wa mazoezi kwenye viwanja vya Mo Bunju Arena ikiwa zimebaki siku mbili kuelekea mchezo huo na kuahidi kucheza kwa morali kubwa

“Tupo na morali kubwa kwenda kwenye mchezo unaofuata licha ya kupoteza kwenye mchezo uliopita kwa mabao ambayo sio machache ila tutakwenda kupambana ili tupatae matokeo tuweze kusonga mbele.” Alisema Bocco

Aidha nahodha huyo aliongezea kuwa wao kama wachezaji wanajiaminisha kutoka na matokeo kwenye mchezo na kutokata tamaa ndani ya dakika 90.

“Tumejiweka na moyo mkubwa, kutokata taamaa na kujiaminisha kuwa tutakwenda kupata matokeo na tutaingia kwenye dakika 90 tukijua tulifungwa mchezo uliopita na tunahitaji kushinda.” Aliongezea Bocco

Kwenye mchezo huo Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Afrika (CAF) limeruhusu Simba kuingiza Uwanjani mashabiki 10,000 kutokana na tahadhari za mlipuko wa ugonjwa wa Corona.

Ili Simba iweze kusonga mbele kwenye hatua ya nusu fainali inahitajika ushindi wa kuanzia mabao 5 na kuendelea bila ya nyavu zao kutikiswa.

error: Content is protected !!