May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Bocco nae asalia Simba, asaini mkataba mpya

Spread the love

 

UONGOZI wa klabu ya Simba umemalizana na nahodha wa kikosi hiko John Bocco kwa kumsainisha mkataba mpya mara baada yaw a awali kumaliza mwisho wa msimu wa 2020/21. Anaripotio Kelvin Mwaipungu..

Dakika chache mara baada ya kumsainisha beki wa kushoto Mohammed Hussein, kupitia ukurasa wa Instagram wa klabu hiyo uliweka picha ilionesha nahodha huyo akisaini mkataba mpya kuendelea kukipiga klabuni hapo.

Licha ya kuweka picha hiyo lakini bado haijajulikana Bocco amesaini mkataba wa muda gani na thamani yake haikuwa wazi.

Nahodha huyo kwa sasa kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara amepachika jumla ya mabao 10 na kutoa pasi mbili za mabao (assist) na kuwa amehusika katika mabao 12 kati ya 58 yaliyofungwa na klabu hiyo mpaka sasa.

error: Content is protected !!