March 4, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Bobi Wine amnyima usingizi Museven

Bobi Wine

Spread the love

Bobi Wine mwanamuziki wa miondoko ya pop na mwanasiasa wa upinzani nchini Uganda, anamnyima usingizi rais wan chi hiyo Yower Museven. Inaripoti mitandao ya kimataifa…(endelea).

Rais Museven yupo kwenye harakati ya kuhakikisha Bobi Wine ambaye jina lake halisi ni Robert Kyagulanyi Ssentamu hapati wasaa wa kukutana na waganda wenye uwanja wa siasa na muziki.

Dhamira ya serikali ya Museven imedhihiri jana baada ya kumkatalia kufanya tamasha lake leo lililopangwa kufanyika jana Disemba 26. Aliyetoa marufuku ya onesho hilo alikuwa Emilian Kayima, msemaji wa Jeshi la Polisi nchini humo.

Sababu iliyotolewa ni kwamba, Bobi Wine hakufuata utaratibu wa kisheria wa kuandika barua ya kuomba ruhusa ili aweze kufanya tamasha hilo.

Hata hivyo, gazeti la Daily Monitor la nchini Uganda liliandika kuwa, mapema leo jana Bobi Wine aliandika kwenye mtandao wa kijamii kuwa, kikosi cha usalama kimevamia tamasha lake la ‘One Love Beach in Busabala’na kuwakamata wafanyakazi wake.

Mwanzoni mwa mwezi Novemba mwanamziki huyo aliruhusiwa kufanya tamasha lake la kwanza kwa sababu lilikuwa la kiburudani na halikuwa la kisiasa.

Maelfu ya watu waliohudhuria tamasha hilo walivaa nguo nyekundu, rangi inayohusishwa na vuguvugu za Bobi Wine. Na pale alipopanga tamasha la pili, serikali imeamua kuzuia.

error: Content is protected !!