March 6, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Boban kuanza kuitumikia Yanga leo

Haruna Moshi Boban, alipokuwa anaitumikia African Lyon

Spread the love

BAADA ya kusajiriwa kwenye dirisha dogo la usajiri kutokea klabu ya African Lyion mchezaji Haruna Moshi ‘Boban’ (31) leo amejumuishwa kwenye kikosi cha Yanga kitakachoanza kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho ‘FA’ dhidi ya Tukuyu Stars kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Anaripoti Kelvin Mwaipungu … (endelea).

Boban ambaye amesajiliwa kwa mkataba mfupi wa miezi sita tu wenye thamani ya Sh. 25 milioni, alifanikiwa kumvutia Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera kwenye baadhi ya michezo ya Ligi Kuu hivyo na kuwaomba viongozi wa klabu hiyo kumsajili.

Mchezo huo wa leo utakuwa nduo wa kwanza kwa Yanga kuanza kuusaka ubingwa wa michuano hiyo ambayo bingwa atafanikiwa kuiwakilisha nchi kwenye Kombe la Shirikisho Afrika katika msimu ujao wa kimashindano.

error: Content is protected !!