Wednesday , 8 February 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Bloomberg Media yazindua mafunzo uandishi habari za fedha Tanzania
Habari Mchanganyiko

Bloomberg Media yazindua mafunzo uandishi habari za fedha Tanzania

Spread the love

TAASISI ya Bloomberg Media Initiative Africa (BMIA) imetangaza kuanza kwa awamu ya pili ya programu ya mafunzo ya uandishi wa habari za masuala ya fedha (FJT) kwa waandishi nchini Tanzania. Mafunzo hayo yamelenga kuwawezesha jumla ya waandishi wa habari 50 wa masuala ya fedha na biashara kuandika habari za kina zinazohusu sekta hizo. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Awamu hiyo ya pili inafanyika baada ya mafunzo hayo kusimama kwa miaka miwili kutokana na changamoto za ugonjwa wa UVIKO-19.

Mafunzo hayo yanaendeshwa kwa ushirikiano kati ya Shule Kuu ya Biashara ya Strathmore ya nchini Kenya, Shule Kuu ya Biashara ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Shule Kuu ya Habari na Mawasiliano ya Umma ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam.

Kurejewa kwa mafunzo hayo kunatokana na mafanikio makubwa yaliyopatikana katika awamu ya kwanza iliyofanyika 2019 ambapo waandishi wa habari 40 walipata taaluma mbalimbali kuhusiana na uandishi wa habari za masuala ya fedha na biashara. Katika awamu ya pili kutakuwa na waandishi wa habari 50 kutoka vyombo vya serikali, sekta binafsi, taasisi zisizokuwa za kiserikali na vyombo vikubwa vya habari.

Pia imeelezwa kuwa mafunzo hayo ya miezi sita yatahusisha mada mbalimbali zikiwamo uchambuzi wa data, masoko ya hisa, uhasibu, sera, uchumi na hivyo kuwezesha mabadiliko ndani ya vyombo vya habari ya namna ya kuandika habari za masuala ya fedha na biashara.

Mafunzo hayo yatatolewa na waandishi wa habari wa Bloomberg News na shule zilizotajwa. Mafunzo hayo yamelenga kuhakikisha kwamba kunakuwa na uwajibikaji, uwazi na utawala bora.

Mafunzo hayo ni sehemu muhimu ya BMIA kuchangia maendeleo katika uandishi wa habari za fedha na biashara barani Afrika, kwa kutambua umuhimu wa vyombo vya habari katika kuleta uwazi, uwajibikaji na utawala bora.

Akizungumzia mafunzo hayo Mkurugenzi  BMIA, Erana Stennett, alisema: “Tumefurahishwa na kurejea tena katika kutoa mafunzo ya programu baada ya miaka miwili. Tunaamini kwa kuwapa waandishi wa habari ujuzi na maarifa ili kuripoti vyema masuala ya biashara na fedha tunachangia ukuaji wa uchumi na maendeleo ya Tanzania.”

Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Profesa Florens Luoga akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uzinduzi wa awamu ya pili ya mafunzo ya uandishi wa habari za uchumi (FJT) nchini Tanzania. Mafunzo hayo yanaratibiwa na Shirika la Bloomberg Media Initiative Africa (BMIA).

Akizungumza katika uzinduzi huo, Gavana wa Benki Kuu (BoT) Profesa Florens Luoga alisema: “Katika kipindi hiki kigumu baada ya janga la corona, uandishi thabiti wa habari za kibiashara na kiuchumi ni msingi mkubwa wa kuweza kuwafahamisha wadau ili kuweza kuwa na msukumo mkubwa wa ukuaji wa uchumi.

“Kwa kutoa mafunzo kwa wanahabari zaidi, BMIA inachangia maendeleo ya kiuchumi ya Tanzania.”

Kuzinduliwa kwa awamu ya pili nchini kunafuatia kuwapo kwa mafanikio makubwa ya programu hiyo kwa nchi za Kenya, Nigeria, Afrika Kusini, Ghana, Zambia, Ivory Coast na Senegali, ambapo zaidi ya waandishi 600 wamepatiwa mafunzo hayo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Washindi saba safarini Dubai NMB MastaBata ‘Kote Kote’

Spread the loveKAMPENI ya kuhamasisha matumizi ya Mastercard na QR Code ‘Lipa...

Habari Mchanganyiko

Bodi ya Maji Wami Ruvu kuchimba visima 10 kupunguza uhaba maji mikoa mitatu

Spread the love  BODI ya Maji ya Bonde la Wami Ruvu imesema...

Habari Mchanganyiko

NBC Dodoma International Marathon kutimua vumbi Julai 23

Spread the loveBENKI ya Taifa ya Biashara (NBC) imetanganza msimu wa nne...

Habari Mchanganyiko

NMB wadhamini wiki ya usalama barabarani

Spread the loveBENKI ya NMB ni miongoni mwa wadhamini wa Wiki ya...

error: Content is protected !!