January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Blatter, Platini watupwa jela miaka nane

Spread the love

KAMATI ya Maadili ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (Fifa) limewafungia kutojihusisha na na mpira wa miguu kwa kipindi cha miaka nane, aliyekuwa Rais wa shirikisho hilo, Sepp Blatter na Mwenyekiti wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Ulaya (UEFA), Michel Platini.

Maofisa hao wamepatikana na hatia ya ukiukaji wa maswala mbalimbali kama vile kashfa ya dola milioni mbili za malipo yasiyo rasmi ambazo zilikabidhiwa kwa Platini mwaka 2011.

Pamoja na maafisa hao wawili kukana mashtaka hayo, lakini kamati hiyo imewatia hatiani na adhabu hiyo inaanza mara moja kuanzia sasa.

Rais huyo wa Fifa tangu mwaka 1998, Bwana Blatter, mwenye umri wa miaka 79, tayari ametangaza kujiondoa katika kinyanganyiro cha kumtafuta rais mpya wakati wa uchaguzi mkuu wa shirikisho hilo mwezi Februari mwakani.

Naye nahodha wa zamani wa Ufaransa Platini, mwenye umri wa miaka 60, na ambaye alionekana kama kiongozi wa baadaye wa shirikisho hilo, amekuwa akipigiwa upatu wa kurithi mikoba ya Blatter katika uchaguzi mkuu ujao. Platini amekuwa Rais wa UEFA tangu mwaka 2007.

Adhabu hiyo iliyotolewa na kamati ya maadili inakatiza maisha ya soka ya maofisa hao waliojitengenezea majina makubwa katika ulimwengu wa mpira wa miguu.

Blatter amesema kuwa atakwenda katika mahakama ya maswala ya michezo (Court of Arbitration for Sport) iliyoko Lausanne kukata rufaa.

Blatter anasema kuwa malipo hayo yalikuwa ya kazi aliyomfanyia lakini kamati ya uadilifu na nidhamu ya FIFA imewapata na hatia ya kuwa yalikuwa malipo ya kiinua mgongo.

Kamati ya uadilifu na nidhamu hata hivyo imewapata na hatia ya kutoa pesa na kuingia katika kandarasi kinyume na maadili ya FIFA.

error: Content is protected !!