Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Biteko aeleza faida marekebisho sheria ya madini
Habari za Siasa

Biteko aeleza faida marekebisho sheria ya madini

Madini ya dhahabu
Spread the love

 

WAZIRI wa Madini Dotto Biteko amesema serikali imekuwa ikifanya jitihada za kubadilisha sheria ya madini ili kuliwezesha Taifa kunufaika na rasilimali hiyo ya madini. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma …  (endelea).

Biteko ametoa kauli hiyo leo tarehe 5 Novemba mwaka huu wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya maendeleo ya sekta ya madini tangu Tanganyika ipate Uhuru mwaka 1961 hadi sasa.

Amesema licha ya Tanzania kujaliwa rasilimali hizo haikunufaiki kutokana na sheria ambazo zimerithiwa kutoka kwenye ukoloni.

Amesema sheria ambazo zilikuwa zikitumiwa wakati wa ukoloni zilikuwa zinamfanya mchimbaji mdogo na mzawa kuonekana mchimbaji haramu na kumfanya mchimbaji mgeni kuwa halali.

“Katika kuendelea kurekebisha sheria ya madini kwa sasa imempa mchimbaji mdogo kuwa na thamani na kunufaika na uchimbaji wa madini,” amesema.

Waziri wa Madini, Doto Biteko

Akizungumzia historia ya uchimbaji wa madini nchini amesema kabla ya uhuru hadi kufikia sasa tunapoadhimisha miaka 60 ya Uhuru, sekta ya madini imepitia katika hatua na miundo mbalimbali ya Serikali.

Amesema pamoja na mambo mengine sekta ya madini imekuwa ikilalamikiwa zaidi kuliko sekta nyingine.

“Kutokana na hali hiyo tangu wakati huo, nyenzo za usimamizi sekta ikiwa ni pamoja na Sera na Sheria ya Madini zimekuwa zikifanyiwa marekebisho na maboresho ya mara kwa mara kulingana na uhitaji wa kufanya hivyo.

“Kwa mfano, mwaka 2009 Serikali ilitunga upya Sera ya Taifa ya Madini na kufuatiwa na Sheria ya Madini ya Mwaka 2010.

“Baada ya kuonekana kwa changamoto kadhaa, Serikali ilifanya mapitio ya Sheria ya Madini 2010 kwa lengo la siyo tu kuimarisha uwezo wa Serikali kuisimamia sekta ili iongeze mchango wake katika Pato la Taifa, bali pia kwa lengo la kuimarisha ushiriki wa wachimbaji wadogo kwenye shughuli za madini.

“Pia kuinua sekta ndogo ya uchakataji madini na kufungamanisha sekta ya madini na sekta nyingine za uchumi kwa maendeleo ya Taifa”amesema.

Amesema mabadiliko sheria hiyo pia yalilenga kutambua haki ya ushiriki wa Serikali katika shughuli zote za uchimbaji, uchakataji na uchenjuaji wa madini na umiliki wa hisa kwa asilimia 16 katika makampuni ya uchimbaji.

Pia Serikali kuwa na uwezo wa kuongeza ushiriki mpaka kufikia asilimia 50 kupitia thamani ya vivutio vya uwekezaji na kikodi alivyopewa mwekezaji.

Akizungumzia mafanikio amesema Serikali imefanya jitihada kuhakikisha watanzania wananufaika na rasilimali madini, huku ikishuhudiwa ongezeko la kasi ya ukuaji wa sekta ya madini.

“Kwa mfano, sekta madini ilikua kwa asilimia 17.7 mwaka 2019 na kuwa ya kwanza kwa ukuaji nchini ikilinganishwa na kipindi cha nyuma kabla na baada ya uhuru.

“Kwa upande wa mchango wa sekta ya madini katika Pato la Taifa uliongezeka kutoka asilimia 3.4 mwaka 2015 hadi kufikia asilimia 5.2 mwaka 2019,’ amesema.

Amesema kabla ya kipindi hicho wastani wa mchango wa sekta kwenye pato la Taifa ulikuwa takribani asilimia tatu.

Aidha, mchango wa sekta katika pato la Taifa uliongezeka hadi kufikia 6.7 mwaka 2020 kutoka 4.8 mwaka 2017.

“Wakati Mchango wa wachimbaji wadogo wa dhahabu kwenye makusanyo ya maduhuli ya Serikali umeongezeka kutoka asimia 10 mwaka 2017/18 hadi kufikia asilimia 27 mwaka 2020/21.

“Katika mwaka 2020 Sekta ya Madini ilichangia asilimia 6.7 kwenye Pato la Taifa, hivi karibuni mchango wa sekta umeongezeka hadi kufikia asilimia 7.7 katika robo ya pili mwaka 2021 (Aprili – Juni),” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!