Spread the love

WAZIRI wa Madini Dotto Biteko amefanya ziara ya kushtukiza katika ofisi ya kuchenjua madini iliopo eneo la Kizota mkoani hapa na kubaini madudu yanayofanywa na wafanyakazi wake, huku Katibu Mkuu akimsimasha Afisa Madini wa Ashen Daniel ili kupisha uchunguzi. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Moja ya madudu ambayo yanafanywa na wafanyakazi wa ofisi hiyo ni kutokujaza gramu za dhahabu zinazoletwa kuchenjuliwa na raia ili zikauzwe sehemu husika.

Akizungumza katika ziara hiyo Waziri Biteko alisema Ofisa Madini Ashen ameshindwa kujaza kwa makusudi gramu za dhahabu ambazo zimeletwa kuchenjuliwa ili wazifanyie utaratibu mwingine wa kuliibia taifa kujaza gramu jambo ambalo ni kinyume na utendaji wa kazi ambao ameagizwa na serikali.

Alisema Ofisa huyo atakuwa mfano kwa wengine, wote wanaofanya kazi kwa kuiibia serikali hawatakuwa katika mikono salama kutokana na kwamba atakwenda nao sambamba na hili zoezi ni endelevu.

Aidha alisema lengo ni kuhakikisha wezi wote wa madini wanaondoka ili kuiacha sekta hiyo ikiwa salama.

Hata baada ya kumbaini Afisa madini huyo, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo kumsimamisha Afisa madini Ashen Daniel kutokana na kushindwa kujaza gramu halisi za dhahabu aliyopima na badala yake kukuta kitabu kipo wazi ilihali wamechenjua madini.

Akihojiwa Daniel alisema ni kweli amepima madini lakini hakujaza kutokana na changamoto mbalimbali ambazo pia alishindwa kuziainisha mbele ya Waziri Biteko na kupelekea kusimamishwa kazini ili kupisha uchunguzi uendelee kuhusiana na kitendo hiko anachofanya.

Alisema Afisa huyo atakuwa mfano kwa maafisa wengine kutokana na utendaji mbovu wa kazi ya madini jambo linalopelekea upotevu mwingi wa madini ambayo yanauzwa bila kujulikana sehemu wanayopelekea.

Mbali na hivyo alimwagiza Afisa Madini wa mkoa kupeleka kazi zake zote za madini za miezi sita ambazo zimefanywa zikiwemo za kuchenjua na uuzaji unaofanywa na wanunuzi wa madini balimbali ambao wamebainika walikuwa wakifanya kazi hiyo bila ya kuwa na leseni lakini waliruhusiwa kufanya kazi hiyo.

Mbali na hilo Katibu wa Wizara ya Madini, Prof. Simon Msanjila amemsimamisha Afisa huyo kwa muda usiojulikana ili kupisha uchunguzi uendelee kutokana na vitendo wanavyofanya katika ofisi hizo, ikiwemo kutofuatilia watu wanaonunua madini bila kuwa na leseni.

“Kuanzia leo nakusimamisha kazi ili uwache watu wafanye uchunguzi kubaini ukweli wa mambo,” alisema Profesa Msanjila.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *