Wednesday , 8 February 2023
Home Kitengo Michezo Bishara united mguu sawa kuwavaa walibya, kumkosa nahodha wao
Michezo

Bishara united mguu sawa kuwavaa walibya, kumkosa nahodha wao

Spread the love

 

UONGOZI wa klabu ya Soka ya Biashara United kutoka mkoani Mara, umesema kikosi chao kipo tayari kwa ajili ya mchezo wa kombe la Shirikisho Barani Afrika dhidi ya Al Alhly Tripoli ya kutoka nchini Libya. Anaripoti Wiston Josia…(endelea)

Mchezoa huo wa mzunguko wa kwanza, utapigwa kwesho kwenye dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam, majira ya saa 9 Alasiri.

Akizungumza na MwanaHALISI Online, Afisa Habari wa klabu hiyo Ben Bago amefunguka kuwa, maandalizi yamekamilika na timu ilikuwa ikifanya mazoezi kwenye Uwanaj wa Uhuru, jijini Dar es Salaam

“Mandalizi yapo vizuri, tupo hatua za mwisho na timu inafanya mazoezi kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.” Alisema Afisa Habari huyo

Kuelekea mchezo huo, tayari klabu ya Soka ya Al Alhly Tripoli Wapo nchini, mara baada ya kuwasili siku ya Jumatano Alfajiri Tarehe 13 Oktoba 2021.

Aidha msemaji huyo aliongezea kuwa, kuelekea mchezo huo watakosa huduma ya nahodha wao Abdulmajid Mangala, ambaye jina lake halikutumwa kwenye Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF), kufuatia kuchelewa kwa usajili wake.

“Nahodha wetu Mangala hatocheza kutokana na jina lake kutopelekwa Caf, kutokana na kuchelewa kusaini mkataba wake mara baada ya kutoka kwenye majairibio nje ya nchi.” Aliongezea

Wapinzani hao wa Biashara United, ni moja ya klabu kongwe, ambayo inamiaka 70 toka kuanzishwa kwake tofauti na Biashara United ikiwa haiizdi miaka 35, toka kuanzishwa kwake.

 

 

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

GGML: Uwanja mpya wa Geita Gold FC kukamilika Mei, 2023

Spread the loveUWANJA wa Magogo unaojengwa na Halmashauri ya Mji wa Geita...

Michezo

Wanafunzi chuo Mwalimu Nyerere wapongezwa kwa ushindi

Spread the love  UONGOZI wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA)...

Michezo

Arsenal waipopoa Manchester United

Spread the loveKLABU ya Arsenal inayoshiriki Ligi Kuu England imewatandika Mashetani Wekundu...

Michezo

Mchezaji Singida apoteza maisha mazoezini

Spread the love  MCHEZAJI na kapteni wa timu ya vijana ya Singida...

error: Content is protected !!