Friday , 3 February 2023
Home Kitengo Michezo Biriani Ulaya; Messi, Ronaldo chaliii!
Michezo

Biriani Ulaya; Messi, Ronaldo chaliii!

Spread the love

 

PAZIA la michuano ya Klabu Bingwa Ulaya limefunguliwa rasmi tarehe 14, 15 Septemba mwaka huu na kushuhudia mastaa namba moja duniani, Lionel Messi na Cristiano Ronaldo ambao wamezichea timu walizosajiliwa kwa mara ya kwanza, wakishindwa kuzipatia pointi tatu katika mechi za awali. Anaripoti Hunda Mintanga TUDARCo … (endelea).

Ronaldo ambaye amesajiliwa na Manchester United kutoka Juventus alishuhudia mashetani hao wekundu wakiangukia pua kwa bao 2-1 kutoka kwa vijana wa Young Boys (Uswiss) ilihali Messi ambaye amechomoka kutoka Barcelona kuelekea PSG ya Ufaransa jana tarehe 16 Septemba aliambulia sare ya 1-1 kutoka kwa Club Brugge (Ubelgiji).

Manchester United waliopo kundi F katika mchezo huo wa kwanza tarehe 14 Septemba, Ronaldo alifungua dimba kwa bao pekee kabla ya Young Boys kuondoka na ushindi.

Jana tarehe 15, PSG walio kundi A nao walibanwa mbavu licha ya kumchezesha Messi ambaye ni kipenzi cha wapenda soka wengi duniani.

Matokeo ya michezo mingine ni kwamba Manchester City wakiwa nyumbani Uingereza wamepata ushindi mnono wa bao 6-3 dhidi ya RB Leipzig, Atletico Madrid 0-0 FC Porto ya Ureno, Liverpool 3-2 AC Milan, Sporting 1-5 Ajax, Inter Milan wakiwa nyumbani pia walipoteza kwa kukubali kipigo cha goli moja kutoka kwa Real Madrid.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

GGML: Uwanja mpya wa Geita Gold FC kukamilika Mei, 2023

Spread the loveUWANJA wa Magogo unaojengwa na Halmashauri ya Mji wa Geita...

Michezo

Wanafunzi chuo Mwalimu Nyerere wapongezwa kwa ushindi

Spread the love  UONGOZI wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA)...

Michezo

Arsenal waipopoa Manchester United

Spread the loveKLABU ya Arsenal inayoshiriki Ligi Kuu England imewatandika Mashetani Wekundu...

Michezo

Mchezaji Singida apoteza maisha mazoezini

Spread the love  MCHEZAJI na kapteni wa timu ya vijana ya Singida...

error: Content is protected !!