May 20, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Bill Gates, mkewe Melinda wafika tamati

Spread the love

 

SAFARI ya miaka 27 katika maisha kati ya tajiri namba nne duniani – Bill Gets na mkewe Melinda, hatimaye imetamatika. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Makubaliano ya kutengana kwa wanandoa hao wawili, yamewekwa hadharani huku wakisisitiza, walipofika hawawezi tena kuishi pamoja.

Katika ujumbe wao kupitia mtandao wa twitter, wameieleza dunia kwamba uamuzi huo ulianza kwa tafakari nzito na hatimaye kufikia uamuzi wa kutalikiana.

Ujumbe wao unaeleza “hatuamini tena kama tunaweza kuwa pamoja kama wanandoa. Baada ya kufikiria sana na kufanya kazi nyingi juu ya uhusiano wetu, tumefanya uamuzi wa kumaliza ndoa yetu.”

Kwa mara ya kwanza, Bill na Melinda walikutana mwaka 1987 pale Melida alipojiunga na kampuni ya tajiri huo – Microsoft. Katika miaka 27 ya ndoa yao, wawili hao wamefanikiwa kupata watoto watatu.

Moja ya mambo makubwa waliyofanya wakiwa pamoja ni uanzishwaji wa wakfu – Bill & Melinda Gates, taasisi hiyo imekuwa ikitumia mabilioni kufadhili kampeni mbalimbali ikiwemo magonjwa ya kuambukizana na kuhamasisha chanjo kwa watoto.

Kulingana na jarida la Forbes, Bill ana utajiri wenye thamani ya Dola za Marekani bilioni 124.

Safari ya utajiri wake ilianza miaka ya 1970, baada ya kufungua kampuni ya Microsoft, kampuni kubwa ya programu ulimwenguni.

“Tunaendelea kuwa na imani ya pamoja katika lengo hilo na tutaendelea kufanya kazi pamoja kwenye wakfu wetu, lakini hatuamini tena tunaweza kukua pamoja kama wanandoa katika sehemu inayofuata ya maisha yetu,” imeeleza taarifa yao kupitia twitter.

Melinda alijiunga na Kampuni ya Microsoft kama msimamizi wa bidhaa mwaka 1987. kwenye moja ya majukumu yake, alikaa pamoja kwenye dhifa ya chakula cha jioni cha biashara mwaka huo huko New York, Marekani.

Akizungumzia namna ilivyokuwa, Bill anasema wawili hao walikuwa wakipendana na kujaliana kwa kiwango cha juu, na kwamba aliamini chochote kinaweza kutokea.

Kwa upande wa Melinda, alisema alikuwa mtu wa kawaida kabisa wakati anaanza kuwa na husuiano wa kimahaba na Bill.

Bill na Melinda walifunga ndoa katika Kisiwa cha Lanai, Hawaii mwaka 1994.

Katika kisiwa hicho, Bill na timu yake walikodi helikopta zote za eneo hilo ili kuzuia wageni wasiohitajika kuruka na helkopta hizo na kuhudhuria sherehe yao bila mwaliko, lakini sawa wawili hao sio wana ndoa tena.

error: Content is protected !!