Friday , 29 March 2024
Home Kitengo Michezo Bilioni nne yajenga Uwanja wa Mpira Kinondoni
Michezo

Bilioni nne yajenga Uwanja wa Mpira Kinondoni

Amos Makala, Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam
Spread the love

MKUU wa mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla ameishukuru Serikali chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kuidhinisha kiasi cha shilingi bilioni nne kwa ajili ya ujenzi wa Uwanja wa Mpira wa Miguu katika eneo la Mwenge, Kinondoni jijini Dar es Salaam. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Makalla ameyasema hayo jana Disemba 5, mwaka huu katika hafla ya ufunguzi wa Barabara ya Morocco – Mwenge, katika Uwanja wa chuo cha Ustawi wa Jamii Kijitonyama.

Wakati akitoa neno kwenye hafla hiyo, Makalla alionekana kutoa shukrani kwa Rais Samia kwa serikali yake kukubali kutoa kiasi hiko cha fedha kwa ajili ya mradi huo wa Uwanja.    

“Tunashukuru kwa kuidhinisha fedha hapa kinondoni kwenye jimbo la Tarimba, kwa miradi mikuu mitatu, mradi wa kwanza ni wa Uwanja wa mpira wa kisasa hapa mwenge ambao unakwenda kujengwa.” Alisema Makalla

Ujenzi wa Uwanja huo ulianza mwaka 2020, mara baada ya kusainiwa mkataba wa makubaliano ya ujenzi kati ya Almashauri ya Kinondoni iliyowakilishwa na Meya Benjamin Sitta, pamoja na Jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) uliowakilishwa na Luten Kanali David Luoga.

Mkataba huo ulisaniwa Januari 27, 2020 na Uwanja huo utakuwa na uwezo wa kuchukua mashabiki 20,000 na pia utakuwa na maduka 50 ndani yake sambamba na mabweni kwa ajili ya kuishi wachezaji.

Aidha mkuu huyo wa mkoa hakuishia hapo aliendelea kusema kuwa mradi huo mpaka sasa umefikia pazuri mara baada ya kutembelea eneo hilo.

“Huo uwanja wa mpira utaghalimu zaidi ya bilioni 4, mimi nilikewenda kutembelea ni mradi mzuri na wamefikia pazuri” alisema Makalla

Uwanja huo ukikamilika utakuwa ukitumiwa na klabu ya Kmc inayoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara kama Uwanja wao wa nyumbani kutokana na timu hiyo kuwa chini ya Manispaa ya Kinondoni.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Makala & UchambuziMichezo

TFF kuamua hatima ya Amrouche

Spread the loveHATIMA ya Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Adel Amrouche kuendelea...

Habari za SiasaMichezo

Matinyi: Dk. Ndumbaro alifanya utani ukaguzi mechi za Yanga, Simba

Spread the loveMsemaji Mkuu wa Serikali, Mobhare Matinyi amesema kauli iliyotolewa na...

Michezo

Gethsemane Group Kinondoni (GGK) waachia video ya Bwana Wastahili

Spread the loveWAIMBAJI maarufu nchini kutoka Gethsemane Group Kinondoni (GGK)SDA wameachia video...

BiasharaMichezo

Gamondi kocha bora mwezi Februari, NBC yamjaza manoti

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) ambae ni mdhamini Mkuu...

error: Content is protected !!