May 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Bilioni 63 zakusanywa tozo miamala ya simu

Dk. Mwigulu Nchemba, Waziri wa Fedha na Mipango

Spread the love

 

SERIKALI imesema tangu tozo za miamala ya simu ianze kukusanywa tayari zimepatikana Sh. 63 bilioni hadi kufiki tarehe 30 Agosti, mwaka huu. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Pia fedha hizo tayari zimeshapelekwa kufanya kazi ambapo jumla ya vituo vya afya 220 vimeanza kujengwa katika tarafa zote zisizokuwa na vituo vya afya nchini.

Taarifa hiyo imetolewa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Mwigulu Nchemba leo tarehe 1 Septemba 2021 wakati akizungumza na waandishi wa habari kutoa ufafanuzi kuhusu tozo mbalimbali zilizoanzishwa na Serikali.

Amesema hakuna tarafa yoyote nchi nzima ambayo haitakuwa na kituo cha afya kwasasa.

“Kodi yetu imeleta matokeo, Watanzania tutembee kifua mbele kwa kujenga nchi yetu wenyewe,” amesema.

Pia amesema watu milioni 30 wanaofanya miamala ya Sh 1 hadi Sh 999 kwa siku  hawakukatwa tozo ya kutuma na kutoa fedha.

“Tumeachia miamala zaidi ya milioni 29 kwa watu ambao wanatumiana kuanzia shilingi moja mpaka Sh999, watu wanaotumiana viwango vile tuliiachilia yote ile kwa sababu dira ya rais sio kukusanya hela tu anaangalia na ustawi wa jamii,  amesema.

error: Content is protected !!