December 9, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Bilioni 5 zatengwa kununua, kukarabati vivuko

Kivuko cha MV Nyerere

Spread the love

Katika kuhakikisha usafiri wa majini unaimarika, serikali imetenga kiais cha Sh. bilioni 5 katika bajeti ya mwaka huu kwa ajili ya  ukarabati  na kununua  vivuko pindi inapohitajika. Anaripoti Moses Mseti, Mwanza… (endelea)

 Imesema pia imetenga Sh. milioni  50 kwa ajili ya ukarabati wa kivuko cha MV Nyerere kilichopinduka  Septemba 20 mwaka jana  wakati kikisafirisha abiria  kutoka Bugorola kwenda Ukara wilayani Ukerewe na kusababisha abiria  230 kufariki  na wengine 41 kuokolewa.

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme nchini (Temesa), Mhandisi Japhet Masele amesema kama wakala wametenga Sh bilioni 5 ambazo ni mapato ya ndani za kukarabati vivuko.

Mhandisi Masele amesema pamoja na fedha za ndani, pia Serikali kuu imekuwa ikitoa fedha kwa Temesa  wakati panapojitokeza kuwapo na shughuli ya ujenzi wa kivuko kipya au ukarabati ikiwa lengo ni moja kuondoa changamoto za vyombo vya usafirishaji abiria na mizigo majini.

“Tunaposema tumetenga Sh bilioni 5 kama fedha za ndani, tayari tumepanga kutengeneza boti mbili  mpya ambapo  moja itapalekwa katika Kisiwa cha Ilugwa  na nyingine tutaangalia palipo na uhitaji wa haraka, kama Serikali tunatambua uwepo wa vivuko  unaongeza uchumi kwa wananchi.

“ vipo vivuko ambavyo  vinaziunganisha nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki(EAC), mfano kivuko cha Kigongo-Busisi ambacho kwanza kinaunganisha mkoa na mkoa, pia  kinatumiwa na nchi za nje.Vile vile kivuko cha Rusumo nacho kinatumika kwa EAC ambapo vyote vinavusha malori ya mafuta,”alisema.

Pia Mhandisi Masele amesema Serikali muda wowote itasaini mkataba  wa ujenzi wa kivuko cha kipya cha Bugorola-Ukara ambacho kitakuwa  mbadala wa MV Nyerere iliyopinduka Septemba 20, mwaka jana na kusababisha vifo.

 

error: Content is protected !!