Wednesday , 8 February 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Bilioni 42 kulipa fidia wananchi Chalinze
Habari za Siasa

Bilioni 42 kulipa fidia wananchi Chalinze

Ridhiwani Kikwete, Naibu Waziri wa Katiba na Sheria
Spread the love

 

SERIKALI ya Tanzania imesema, Sh.42.3 bilioni zimetengwa ili kulipa fidia kwa wananchi waliopisha miradi wa kusafirisha umeme kutoka Kinyerezi na Bwawa la Mwalimu Nyerere. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Kauli hiyo, imetolewa leo Jumatatu tarehe 19 Aprili 2021, bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Nishati, Stephen Byabato wakati akijibu swali la Ridhiwan Kikwete, Mbunge wa Chalinze kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

“Je, ni lini Serikali itawalipa fidia wananchi wa Chalinze waliopisha ujenzi wa miundombinu ya miradi ya kusafirisha umeme kutoka Kinyerezi na Bwawa la Mwalimu Nyerere,” ameuliza Ridhiwani

Akijibu swali hilo, Byabato amesema, Serikali kupitia Tanesco, inatekeleza mradi wa ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme ya msongo wa kilovolti 400 kutoka kituo cha kuzalisha umeme cha Julius Nyerere hadi Chalinze na ujenzi wa kituo cha kupoza umeme katika Kijiji cha Chaua – Chalinze.

Bwawa la Umeme Rufiji

Amesema, Serikali kupitia Tanesco, imekamilisha tathimini ya mali za wananchi na taasisi zilizopisha utekelezaji wa mradi huu na fidia kuidhinishwa na mthamini mkuu wa Serikali.

Naibu waziri huyo amesema, jumla ya Sh.42.3 bilioni, zimetengwa katika bajeti ya mwaka 2021/22, kwa ajili ya malipo ya fidia kwa wananchi waliopisha mradi.

Amesema, fidia ya wananchi hao itaanza kulipwa kuanzia Mwaka wa fedha2021/22 baada ya taratibu zote kukamilika.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Bunge labaini madudu mfumo ukusanyaji mapato, h’shauri tatu kikaangoni

Spread the love  KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali...

Habari za Siasa

Mkuu wa wilaya ya Rungwe azindua vyumba sita vya madarasa vya thamani ya 64 mil

Spread the love  MKUU wa Wilaya ya Rungwe, Jaffar Haniu amezindua vyumba...

Habari za Siasa

Mbunge afurahia mabilioni ya Samia kutua jimboni

Spread the love  MBUNGE wa Igunga, Nicholas Ngassa ameishukuru Serikali kwa utekelezaji...

Habari za Siasa

PIC yaishauri Serikali kuanzisha mfuko wa uwekezaji kusaidia mashirika ya umma

Spread the love  KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji...

error: Content is protected !!