November 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Bilioni 328 kugharamia Sensa 2022

Dk. Mwigulu Nchemba, Waziri wa Fedha na Mipango

Spread the love

 

WAZIRI wa Fedha na Mipango, nchini Tanzania, Dk. Mwigulu Nchemba amesema, Sh.328.2 bilioni, zinatarajiwa kutumika kugharamia sensa ya watu na makazi kwa mwaka 2022. Anaripoti Jemima Samwel, DMC…(endelea).

Akiwasilisha bajeti ya Serikali kwa mwaka 2021/22, leo Alhamisi tarehe 10 Juni 2021, bungeni jijini Dodoma amesema, katika historia ya Sensa nchini, Sensa ya Mwaka 2022 itatumia teknolojia ya vishikwambi (tablets) katika utengaji wa maeneo ya kijiografia na ukusanyaji wa takwimu uwandani.

“Matumizi ya teknolojia hii yana manufaa makubwa, hasa katika kupunguza gharama na muda wa kukusanya na kuchakata takwimu, hali inayowezesha kutoa matokeo ya Sensa ndani ya muda mfupi,” ameema Dk. Mwigulu

https://www.youtube.com/watch?v=c5nbVWXuTiw

Amesema, zoezi la Sensa ya Watu na Makazi ni jukumu la kila mtu, “natoa wito kwa kamati zote za Sensa, Wakuu wa Mikoa na Wilaya zote, waheshimiwa Wabunge pamoja na wananchi wote kwa ujumla kuhakikisha wanatoa ushirikiano wa kutosha katika maandalizi ya Sensa na wajitokeze wote siku ya kuhesabu watu.”

“Lengo ni kuhakikisha watu waliolala nchini usiku wa kuamkia siku ya Sensa (usiku wa sensa) wanahesabiwa na kuchukuliwa taarifa zao za kiuchumi, kijamii, mazingira na makazi wanayoishi na mengine mengi kwa ajili ya kupanga mipango endelevu ya maendeleo ya wananchi,” amesema

error: Content is protected !!