Friday , 9 June 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Bilioni 223.9 zapelekwa Tunduru ndani ya miaka 2 ya SSH
Habari za Siasa

Bilioni 223.9 zapelekwa Tunduru ndani ya miaka 2 ya SSH

Spread the love

 

ZAIDI ya Sh. bilioni 223.9 zimepelekwa Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma kusimamia shughuli mbalimbali za maendeleo tangu mwezi Machi 2021 – Machi 2023. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Wakili Julius Mtatiro ameeleza hayo wakati wa Kongamano la Kiwilaya la kuadhimisha miaka miwili ya uongozi wa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan, lililofanyika katika ukumbi wa Cluster wilayani humo.

DC Mtatiro ameeleza kuwa mradi wa kipekee na kihistoria ambao umetia fora ni ule wa Sh. bilioni 150 ambazo zimepelekwa wilayani humo kukamilisha ujenzi wa Msongo Mkubwa wa umeme wa kilovoti 220 kutoka Songea hadi Tunduru wenye urefu wa kilomita 210, mradi ambao utamaliza kabisa matatizo ya umeme wilayani Tunduru na ambao utakamilika ndani ya miezi 15 huku Wakandarasi wakiwa wamesharipoti wilayani humo.

Miradi mingine iliyopeleka fedha nyingi wilayani Tunduru ni Mradi wa Umeme Vijiji (REA), Sh.bilioni 31.9, Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Sh. Bilioni 9.6, Barabara Vijijini Sh.Bilioni 8, Miundombinu ya Shule za Msingi na Sekondari Sh. Bilioni 7.4, Miundombinu ya Sekta ya Afya Sh. Bilioni 3.1, Miundombinu ya Maji Sh. Bilioni 5.2, Kilimo na Ushirika Bilioni 4.5,  Elimu Bila Malipo Sh.Bilioni 1.5.

DC Mtatiro amewaasa wananchi wa Tunduru kuitunza miundombinu yote inayojengwa wilayani humo na kuitumia kwa faida ya kuendeleza uchumi wa familia na taifa ili kila kizazi kipate manufaa.

DC Mtatiro alisisitiza watumishi wote wa serikali kuendelea kutumia kila shilingi inayofikishwa Tunduru kwa uaminifu mkubwa ili kuleta tija ya muda mrefu na amemshukuru Rais Samia kwa kuwekeza katika wilaya hiyo ya pembezoni mwa nchi fedha nyingi zaidi kuliko awamu zote za serikali za Tanzania.

Akitoa pongezi katika kongamano hilo, Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru Said Bwanali amesema Rais Samia anatimiza Ilani ya Uchaguzi ya CCM ipasavyo na ameitendea haki wilaya hiyo.

3 Comments

  • @THINK/Dedication/Remember”@ EMPLOY THEM ALL – ALL TANZANIAN HAS JOB TO DO

    In 2021, the unemployment rate in Tanzania remained nearly unchanged at around 2.74 percent. With a decline of 0.04 percentage points, there is no significant change to 2020. Over the observed period, the unemployment rate has been subject to fluctuation.

  • Wapambania haki za Binadamu wamebuni Mbinu za Mwanamke kupata SIFA ZINAZOSTAHIZI KWA KUMWEKEA VIKWAZON VYA KILA MTU ANATAKIWA KUMUONA MWANAE ALIYEMZAA (MZEE/kabila ANATAKA URAIS KULE ULIKOENDA KUONA). MHE ULIKOOA KULE KUNA MTU ANATAKIWA KUGAWA NCHI YA TANZANIA KILA MKOA UWE NCHI.. … MHE. KULE ULIKOOA KUNA MTU ANAMAWAZO YA NYERERE TUMECHOKA

    KAMA UNA MATOTO WA KIKE UNAJUA FURSA ULIONAYO KAMA MZAZI

    KAMA UNA MTOTO WA KIUME UNAJUA FURSA ULIYONAYO USIMSAHAU BASH YUPO KULE

  • Wapambania haki za Binadamu wamebuni Mbinu za Mwanamke kupata SIFA ZINAZOSTAHIZI KWA KUMWEKEA VIKWAZON VYA KILA MTU ANATAKIWA KUMUONA MWANAE ALIYEMZAA (MZEE/kabila ANATAKA URAIS KULE ULIKOENDA KUONA). MHE ULIKOOA KULE KUNA MTU ANATAKIWA KUGAWA NCHI YA TANZANIA KILA MKOA UWE NCHI.. …

    MHE. KULE ULIKOOA KUNA MTU ANAMAWAZO YA NYERERE TUMECHOKA…

    MHE. KULE ULIKOOA KUNA JAMBO LETU LA KATIBA MPYA…

    MHE. KULE ULIKOOA HUKUWAELEWA WANATAKA UWE WAZIRI MKUU AJAE…

    ULIKOOA ULIPELEKA NYOTA YA WATU KUSHINDA BIKO KILA SIKU….

    MHE.. KULE ULIKOOA WAMEPEWA KAZI YA KUTULETEA RAIS WA KWANZA MLEMAVU/KUTOKA UPINZANI

    KAMA UNA MATOTO WA KIKE UNAJUA FURSA ULIONAYO KAMA MZAZI

    KAMA UNA MTOTO WA KIUME UNAJUA FURSA ULIYONAYO USIMSAHAU BASH YUPO KULE

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Lussu: Mkataba wa DP bandarini si wa miaka 100

Spread the loveMAKAMU Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, amesema hakuna ukweli wowote...

Habari za SiasaTangulizi

Maulid Mtulia: Kutoka ubunge hadi U-DAS

Spread the love ALIYEKUWA mbunge wa Kinondoni, kupitia vyama vya The Civil...

Habari za Siasa

Lusinde: CCM hatuliachii ng’o jimbo la Moshi Mjini

Spread the loveMJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (NEC), Livingston...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar: Bakharesa hajavamia shamba letu

Spread the love  IKULU Visiwani Zanzibar, imeeleza kuwa eneo la kiwanda cha...

error: Content is protected !!