Tuesday , 26 September 2023
Home Habari Mchanganyiko Bilioni 17 kujenga bandari kavu Tunduma
Habari Mchanganyiko

Bilioni 17 kujenga bandari kavu Tunduma

Spread the love

HALMASHAURI ya mji Tunduma iliyopo wilayani  Momba mkoani Songwe imepatiwa Sh 17 bilioni kutoka serikali kuu kujenga bandari kavu katika mtaa wa Mpemba. Anaripoti Ibrahim Yassin, Songwe …(endelea).
Bandari hiyo inatajwa kuwa itachochea mapato kwa halmashauri na serikali kwa ujumla pamoja na kupunguza msongamano kwenye mpakani wa Tunduma na Nakonde.

Inaelezwa kuwa asilimia 72 ya mizigo inayovushwa kwenye Bandari ya Dar Es salaam kuelekea mpakani Tunduma.

Akizungumza mwishoni mwa wiki, Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo, Philimon Magesa alisema Tunduma ni mji wa kibiashara ambao umekuwa ukielemewa na uwingi wa  magari yanayovusha mizigo kwenda kwenye nchi wanachama wa Jumuiya ya kusini mwa Afrika (SADC) hivyo mikakati ya ujenzi wa Bandari kavu utaongeza mapato kwa Serikali.

Alisema nia ya ujenzi wa Bandari hiyo ni kutanua wigo wa utoaji huduma kwa jamii zote hali itakayoongeza uchumi wa nchi.

Mjumbe wa kamati tendaji kutoka chama cha madereva Tanzania, Mussa Samwel alisema yeye na wenzake kwenye umoja huo wamepata taarifa kuhusu ujenzi wa Bandari hiyo na  kusema kuwa kutokana na umuhimu wake ipo haja serikali kuharakisha ujenzi huo na kutatua changamoto zilizopo za kimpaka ziweze kutatuliwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Rais Samia apewa tano ujenzi barabara Mtwara

Spread the loveWANANCHI wa Mkoa wa Mtwara, wameishukuru Serikali ya Rais Dk....

BiasharaHabari Mchanganyiko

Serikali kununua mitambo 15 ya kuchoronga miamba

Spread the loveSerikali kupitia Wizara ya Madini imepanga kununua mitambo 15 ya...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Mtanzania aweka rekodi kimataifa kwa kiwanda cha kusafisha dhahabu

Spread the loveIMEELEZWA kuwa Kiwanda cha Kusafisha dhahabu cha Geita Gold Refinery...

Habari Mchanganyiko

MAIPAC kusaidia Kompyuta shule ya Arusha Alliance

Spread the loveTaasisi ya Wanahabari ya kusaidia Jamii za pembezoni (MAIPAC) imeahidi...

error: Content is protected !!