August 10, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Bilioni 10 zatengwa kilimo cha mirungi

Spread the love

UHURU Kenyatta, Rais wa Kenya amesema, serikali yake imetenga Dola za Marekani 10 milioni kwa ajili ya kusaidia wakulima wa zao la mirungi.

Akizungumza wakati wa kusaini mswada wa kulitambua zao hilo kisheria ili kukuza pato la Kenya amesema, fedha hizo zitatolewa na Wizara ya Kilimo na kwamba zitatumika kuweka mikakati ya kuzalisha na kusambaza zao hilo.

Kenyatta amefikia uamuzi huo kutokana na kilimo cha zao hilo kudorora kufuatia Ulaya kupiga marufuku uuzwaji wa mirungi katika mataifa yao.

Pia kiongozi huyo amesema, ataunda jopo maalumu la kuangazia changamoto katika sekta ya ukuzaji wa mirungi ambayo itatoa mapendekezo kwa serikali na hatimaye kuchukua hatua.

error: Content is protected !!