June 19, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Bilioni 1 kutatua kero ya maji Ilala

Spread the love

Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, jijini Dar es Salaam imetenga kiasi cha Sh. 1,181,338,150/= ili kuboresha huduma za maji kwa wakazi wake ndani ya kipindi cha mwaka mmoja ujao, anaandika Pendo Omary.

Akizungumza na MwanaHALISI Online leo, Charles Kuyeko, meya wa manispaa hiyo amesema fedha hizo ni sehemu ya utekelezaji wa mkakati wa kuboresha huduma ya maji vijijini kutoka asilimia 67.1 mwaka 2015 hadi asilimia 85 ifikapo mwaka 2020.

“Sambamba na fedha hizo pia ipo miradi mikubwa ya maji inayoendelea katika maeneo ya Kipunguni B mji mpya wenye kisima chenye uwezo wa kuzalisha mita mraba 22 kwa saa, kilichochimbwa na tanki la mita mraba 250 ambapo pumpu imejengwa,” amesema.

Meya Kuyeko ameeleza zaidi kuwa tatizo la maji huenda likapatiwa ufumbuzi wa haraka kwani ukichilia mbali mradi mkubwa wa maji eneo la Kipunguni B lakini pia upo mradi mwingine katika eneo la Kivule wenye uwezo wa kuzalisha mita mraba 24 kwa saa na tanki la mita mraba 150 limejegwa, huku mradi wa maji Bangulo ambao umekamilika ukiwa katika hatua ya majaribio.

“Mpaka sasa, wakazi wanaopata maji safi na salama katika manispaa yetu ni asilimia 72 huku wastani wa umbali wa kupata maji ukiwa ni mita 150 na wakazi wenye maji ya bomba majumbani wakiwa ni asilimia 24, idadi ya visima virefu ni 247 huku visima vifupi vikiwa 69,” amesema.

error: Content is protected !!