Monday , 27 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Bilionea wa Uingereza abambikiwa watoto watatu
Habari Mchanganyiko

Bilionea wa Uingereza abambikiwa watoto watatu

Spread the love

MFANYABIASHARA mashuhuri nchini Uingereza na ambaye anaogelea kwenye utajili wa mamilioni ya dola, Richard Mason (54), “ameingizwa chaka” na mkewe, baada ya kusingiziwa kuwa baba wa watoto wake watatu.

Mason aligundua utapeli huo, baada ya kushindwa kupata mtoto na mke wake wa sasa Emma na hivyo kuamua kwenda kufanyiwa uchunguzi wa kitabibu. 

Hili limefanyika takribani miaka 25 tangu mke wake wa awali Kate, kuzaa watoto watatu – mapacha Ed na Joel (19) pamoja na Willem (23) – na kumuamisha kuwa ni wake.

Anasema, alijadiliana kuhusu suala hilo na Kate, lakini mama huyo amegoma katakata kumtajia baba wa watoto hao.

“Nimekua nikijiuliza ni nani baba ya watoto wangu? Sijaweza kupata jibu. Sikuwahi kuwaza jambo hili. Nilihisi kama mtu aliyemgongwa na nyundo,” ameeleza Mason katika mahojiano yake na kituo cha BBC Radio 5 Live.

Mason anasema kilichomshutua zaidi ni kwamba daktari alimfahamisha kuwa alikuwa na ugonjwa unaofahamika kama Cystic Fibrosis uliomfanya kupoteza nguvu ya kuzalisha tangu alipokua mdogo.

Hali iliyomaanisha kuwa yeye sio baba ya watoto wake watatu aliyodhani amezaa na mke wake huyo wa zamani (Kate).

Anaongeza, “nilifahamishwa kuwa wanaume wote wanaougua cystic fibrosis hawana uwezo wa kuzalisha. Nilidhani pengine nimepewa majibu ambayo si sahihi, lakini daktari alinihakikishia kuwa ana uhakika kuhusu uchunguzi wake na kwamba nahitaji kuzungumza na mtalaka wangu kuhusu baba wa watoto wetu.”

Hata hivyo, uchunguzi wa DNA umekanusha madai hayo.

“Kwa muda mrefu ugunduzi huo umenipatia usumbufu wa kimawazo,”Mason alielezea.

“Nimekua nikijiuliza ni nani baba ya watoto wangu, sikuwaza lingine.”

Richard alimshitaki mtalaka wake kwa utapeli mwezi Novemba mwaka jana na amekubali kumlipa dola 320,000 kwa kumharibia sifa kutokana na dola zaidi ya milioni tano alizolipwa walipoachana.

Kate (mtalaka wa Mason) amekataa kumtaja baba watoto; na kwamba Jaji alimkubalia kutomtambulisha baba wa watoto wake.

Lakini kwa nini Kate ameamua kutomtaja baba halali wa watoto wake? Wakili Roger Terrell, anayemtetea Richard Mason, ameliambia gazeti la Daily Telegraph kuwa  “kwa kweli hatuelewi hilo kabisa.”

Mason anasema, “Kuna wakati vijana hawa watataka kumjua baba yao mzazi – na wakati huo ukifika nitawafahamisha. Sijui kama baba yao ni mmoja wa marafiki wangu wa karibu.

“Huenda ni mtu wa karibu sana na mimi, mawazo hayo hunijia kila nikiwaangalia vijana wangu wakicheza mpira wa miguu au magongo. Kwa kweli sijui.”

Anasema, “ukijipata katika hali kama hii ambayo inaathiri maisha yako kwa kiwango kibwa hivi,bila shaka ungelipenda kumjua mhusika mkuu.”

Mfanyibiashara huyo sasa ameahidi zawadi ya dola 6,400 kwa mtu yeyote atakaemsaidia kubaini baba mzazi wa watoto wake.

“Huenda ni mtu wa karibu sana na mimi, mawazo hayo hunijia kila nikiwaangalia vijana wangu wakicheza mpira wa miguu au magongo. Kwa kweli sijui, anaeleza Richard Mason.

Gazeti la Daily Mail la Uingereza, limeripoti kuwa Mason anaamini watoto wake huenda wamezaliwa na mwanamume ambaye amekuwa na uhusiano wa kimapenzi na mke wake wa zamani miaka ya 1990- alifanya kazi na katika benki ya Barclays, tawi la London ambako Kate alikua akifanya kazi.

Kisa hiki kimemuacha na masikitiko makubwa Mason, baada ya watoto wawili kukatiza mawasiliano nae.

“Naona kile wanachofanya katika mtandao wa kijamii wa Facebook na hilo linanivunja moyo sana. Mkubwa wao alifuzu chuo kikuu siku chache zilizopita na hakuna mtu aliyenialika,” aliliambia gazeti la Daily Mail.

Siku hizi ni Ed, mmoja wa mapacha hao, anaewasiliana na Mason.

Naona kile wanachofanya katika mtandao wa kijamii wa Facebook na hilo linanivunja moyo sana. Mkubwa wao alifuzu chuo kikuu siku chache zilizopita na hakuna mtu aliyenialika.

Lakini wiki iliyopita Joel, pacha wa Ed alivunja kimya chake kwa Daily Mail na kukosoa vikali tabia ya Mason.

”Yeye ni mtu mwenye ubinafsi na sio aina ya mtu ungelipenda kuwa pamoja naye. Nilianza kugundua hilo nilipokua na umri wa miaka 15” alisema.

Kando na hilo kijana huyo amesema hana haja ya kumjua babake mzazi.

“Richard ni baba yangu sina haja ya kumjua baba mwingine. Sidhani hata kama yuko hai.

Habari hii, imepatikana kwa msaada m wa BBC na vyanzo vingine vya habari – mhariri

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kasekenya aipa Tanroads wiki kukarabati barabara Morogoro

Spread the loveNaibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya ametoa wiki moja...

ElimuHabari Mchanganyiko

Rubani mtarajiwa Tusiime awashangaza wazazi

Spread the loveWAZAZI walioshiriki siku ya taaluma na maonyesho ya shule ya...

Habari Mchanganyiko

Wanne wadakwa kwa kusafirisha punda 46 nje ya nchi

Spread the loveJeshi la Polisi kikosi cha kupambana na kuzuia wizi wa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Rais Samia: Tutaendelea kupigania malengo ya afrika

Spread the loveRais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema dhamira ya Tanzania...

error: Content is protected !!