May 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Bilionea Uganda ajitosa kuinunua Chelsea

Joel Jaffer A’ita

Spread the love

 

BILIONEA Joel Jaffer A’ita raia wa Uganda ameibua gumzo baada ya kuwasilisha ombi la kutaka kuinunua Klabu ya Soka ya Chelsea inayoshiriki Ligi Kuu ya England. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Bilionea huyo ambaye ni Mhandisi wa ujenzi kitaaluma ambaye ana Shahada ya Kwanza kutoka Chuo Kikuu cha Makerere, pia anamiliki Klabu ya Michezo ya Arua Hill ya Ligi Kuu ya Uganda.

Aliwasilisha rasmi ombi lake la kuinunua The Blues, na kuwa raia wa pili wa Uganda kutoa zabuni kwa klabu ya soka ya Uingereza baada ya jaribio la Michael Ezra Mulyoowa kufanya hivyo kwa Leeds United mwaka 2004.

“Niko tayari kutwaa Klabu ya Soka ya Chelsea ” A’ita aliiambia Kawowo Sports Media Alhamisi.

A’ita ametoa ofa ya dola bilioni 3.3 kwa bilionea wa Urusi, Roman Abramovich ambaye ni mmiliki wa Klabu hiyo ya Chelsea na anakusudia kuita klabu hiyo ‘Klabu ya Soka ya Kongolo (Kongolo FC)’

“Kufuatia taarifa kwa umma kuhusu nia ya Chelsea FC kuuzwa, ningependa kueleza nia yetu ya kununua klabu. Kwa sasa klabu hiyo ina thamani dola za Marekani 3.2 bilioni (Tsh trilioni 7.4) tutatoa dola bilioni 3.3 (Tsh trilioni 7.6). Tunakusudia kubadili jina la klabu kama Kongolo FC,” Aita aliandika katika barua hiyo kwa Abramovich.

Aita aliingia katika ulingo wa soka nchini Uganda mwaka wa 2019 alipotwaa Klabu ya Soka ya Doves All Stars.

error: Content is protected !!