Wednesday , 8 February 2023
Home Kitengo Michezo Bilionea Patrice Motsepe, rais mpya CAF
Michezo

Bilionea Patrice Motsepe, rais mpya CAF

Spread the love

 

RAIS mpya wa shirikisho la kandanda barani Afrika (CAF), Patrice Motsepe, ameomba umoja wakati akitafuta kurejesha sifa ya shirika hilo. Anaandika Mwandishi Wetu,

Motsepe anachukuwa hatamu za kuliongoza shirikisho linalokabiliwa na matatizo, baada ya Ahmad Ahmad, aliyekuwa rais wa kwanza wa CAF kupigwa marufuku na Shiriko la soka ulimwenguni (FIFA), Novemba mwaka jana.

Hata hivyo, zuwio lake la kutojihuisha na soka kwa miaka mitano kuhusiana na “masuala ya utawala,” limepunguzwa hadi miaka miwili baada ya kukata rufaa kwenye mahakama ya michezo.

Amesema, “Afrika inahitaji busara za pamoja, lakini inahitaji kipaji cha kipekee cha busara za kila rais wa chama cha soka na kila taifa mwanachama.

“Tukifanya kazi pamoja, soka barani Afrika itashuhudia mafanikio na ukuaji ambavyo haijavifaidi katika kipindi kilichopita.”

Motsepe alisema, ameweka msisitizo kwenye kuboresha ufanisi wa timu za Afrika kwenye ngazi ya kimataifa.

Bara hilo limekabiliwa na vizuizi katika miaka ya karibuni ambapo timu zote zilizofuzu kushiriki mashindano ya kombe la dunia 2018 nchini Urusi yaliondolewa kwenye raundi ya makundi.

Aliyekuwa Rais wa CAF Ahmad Ahmad, raia kutoka Madagascar, alipigwa marufuku na FIFA kujihusisha na mpira wa miguu kwa miaka miwili.

Alisema, “mpira wa miguu ni zana yenye nguvu ya kurejesha fahari, heshima na taadhima ya Waafrika, na Afrika inaweza kutoa na kushindana kwa ngazi ya juu kabisaa duniani, katika mashindano yote – ya kombe la dunia na hata ubingwa wa vilabu wa FIFA.”

Alisema, “dunia itatuheshimu wakati timu za Afrika zitakapofanikiwa kimataifa. “Siyo wakati wachezaji wetu bora wanaheshimiwa barani Ulaya – Samuel Eto’o, Didier Drogba, Salah, Mane kutoka Liverpool na George Weah. Tumelifanya hilo. Tunataka timu zetu za taifa kushindana na kushinda na kufanikiwa.”

Wiki chache zilizopita, Motsepe, raia wa Ivory Coast Jacques Anouma; raia wa Mmauritania Ahmed Yahya, na raia wa Senegali, Augustin Senghor walikuwa wanapambania nafasi ya rais.

Jacques Anouma ameteuliwa kuwa makamu wa kwanza wa rais wa CAF.

Lakini mikutano ya wagombea iliyoratibiwa na FIFA nchini Morocco na Mauritania ilimfanya Motsepe kuwa mgombea pekee. Senghor na Yahya walipewa nafasi za makamu wa kwanza na wa pili wa rais.

Anouma, ambaye awali alitangaza makubaliano hayo “kutokuwa ya kidemokrasia,” ni mwanachama wa zamani wa kamati ya utendaji ya FIFA na anakuwa mshauri maalumu wa Motsepe.

Wakati baadhi ya maafisa wa CAF wakilalamikia madai ya uingiliaji wa FIFA, rais wa shirikisho hilo, Gianni Infatino, alipuuza jukumu la shirika lake.

Alisema, “nafurahi kwamba FIFA imeweza kuchangia, hata kama ni kidogo, juu ya wakati huu muhimu wa mpira wa miguu kwenye bara hili adhim.”

Kocha mshindi wa zamani wa kombe la mataifa ya Afrika Claude le Roy alihoji ushiriki wa FIFA katika uchaguzi wa Motsepe, kwa kuzingatia kwamba “hawangethubutu kufanya hivyo barani Ulaya au Amerika Kusini.”

“Infantino, acha mauaji na soka la Afrika … kulaazimisha sheria yako kwa Afrika katika uchaguzi,” Le Roy aliliambia shirika la habari la AFP.

Maafisa wengi wanaamini Infantino tayari alimuunga mkono Ahmad kisiri miaka minne iliyopita, wakati Mmalagasy huyo alipokomesha uongozi wa miaka 29 wa Mcameroon Issa Hayatou.

Lakini baada ya mwanzo wa matumaini, Ahmad alianza kuboronga kuanzia mzozo mmoja hadi mweingine, ambayo hatimaye ilimsababishia kuondoka kwenye urais kwa fedheha.

“Shimo la rushwa na ubinafsi”

FIFA iliingiwa na wasiwasi kuhusu masuala ya utawala ndani ya CAF kiasi kwamba ilimtuma katibu mkuu wake Fatma Samoura mjini Cairo kwa miezi sita kusaidia katika uendeshaji wa shirikisho hilo.

Motsepe ndiye tajiri wa tisa barani Afrika akiwa na utajiri binafasi unaokadiriwa na jarida la Forbes kufikia dola bilioni 2.9. Anamiliki klabu ya washindi ya Ligi ya mabingwa wa CAF mwaka 2015 – Mamelodi  Sundowns.

Gazeti la Afrika Kusini, Daily Maverick, limeripoti kuwa Motsepe anarithi shirika lililoelezwa kama “shimo la rushwa na ubinafsi.”

“CAF inahitaji kujitenga na njia za kizamani zilizochoka, tabia za kimfumo na hisia kwamba inawatumikia wale wanaokaa kwenye kamati ya utendaji, badala ya kinyume cha hilo,” liliandika gazeti hilo.

Issa Hayatou aliiongoza CAF kwa miaka 29 na utawala wake ulifikishwa kikomo na Ahmad Ahmad mwaka 2016.

CAF inamtegemea Motsepe kutumia mahusiano yake ya kibiashara barani Afrika kuvutia wafadhili wapya.

Kampuni ya mafuta ya Ufaransa ya Total ndiyo wafadhali wakuu, lakini undani wa makubaliano ya miaka nane yalioanza 2016 haujawahi kuwekwa wazi.

“Asilimia 95 ya majadiliano yetu yatahusu soka..lakini nataka pia asilimia tano iwe kuhusu utambuzi kwamba soka haliwezi kufaniiwa na kustawi bila ushirikiano na sekta binafsi.

“Tunahitaji ushirika na sekta binafsi ili kufadhili na kuwezesha upatikanaji wa mapato zaidi,” alisema Motsepe.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

GGML: Uwanja mpya wa Geita Gold FC kukamilika Mei, 2023

Spread the loveUWANJA wa Magogo unaojengwa na Halmashauri ya Mji wa Geita...

Michezo

Wanafunzi chuo Mwalimu Nyerere wapongezwa kwa ushindi

Spread the love  UONGOZI wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA)...

Michezo

Arsenal waipopoa Manchester United

Spread the loveKLABU ya Arsenal inayoshiriki Ligi Kuu England imewatandika Mashetani Wekundu...

Michezo

Mchezaji Singida apoteza maisha mazoezini

Spread the love  MCHEZAJI na kapteni wa timu ya vijana ya Singida...

error: Content is protected !!