Sunday , 19 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Bilionea mwingine Tanzania afariki dunia, ni Ali Mufuruki
Habari MchanganyikoTangulizi

Bilionea mwingine Tanzania afariki dunia, ni Ali Mufuruki

Marehemu Ali Mufuruki
Spread the love

MFANYABIASHARA mashuhuri na mmoja wa mabilionea wakubwa nchini, Ali Mufuruki (60), amefariki dunia. Alikuwa akisumbuliwa na homa ya mapafu. Anaripoti Saed Kubenea … (endelea).

Mufuruki anakuwa mfanyabiashara wa pili mkubwa nchini Tanzania, kufariki dunia ndani ya kipindi cha miezi sita. Alikuwa mmoja wa wamiliki wa makampuni kadhaa, ikiwamo Infotech Investment Group Limited. 

Mwingine aliyefariki dunia karibuni kabisa, ni Reginard Mengi, bilionea wa Tanzania, aliyekuwa akimiliki makampuni kadhaa chini kupitia mwamvuli uliopewajina la Industrial Products Promotions (IPP Limited).

Taarifa kutoka ndani ya familia ya Mufuruki zinasema, mfanyabiashara huyo, amekutwa na mauti, usiku wa kuamkia leo, tarehe 8 Desemba 2019, katika hospitali ya Morningside, nchini Afrika Kusini.

Kwa mujibu wa msemaji wa familia, Gilman Kasiga, mfanyabiashara huyo mashuhuri nchini, amekutwa na mauti majira ya saa 10 alfajiri kwa saa za Tanzania, sawa na tisa alfajiri kwa saa za Afrika Kusini.

Anasema, kabla ya kupelekwa Afrika Kusini kwa matibabu, Mufuruki alikuwa amelazwa kwenye hospitali ya Aga Khan, jijini Dar es Salaam. 

Mufuruki ambaye alikuwa mwenyekiti na mwanzilishi wa Jukwaa la Wakurugenzi Watendaji wa Makampuni (Ceo rondtable), 1 Desemba mwaka huu, alijiuzulu wazifa wa Mwenyekiti wa bodi ya kampuni ya Vodacom Tanzania. 

Katika kipindi cha uhai wake, mbali ya kuwa mwenyekiti mwanzishi wa wakurugenzi watendaji wa makampuni – Founding Chairman of CEO Roundtable of Tanzania – amekuwa kiongozi katika taasisi ALI – Africa  Leadership Initiative – katika eneo la Afrika Mashariki.

Mufuruki anatajwa na baadhi ya mitandao ya kijamii ulimwenguni, kuwa anaogelea katika utajiri wa kitita cha dola za Marekani 110 milioni.

Hata hivyo, Mufuruki hayumo kwenye orodha ya wafanyabiashara matajiri wakubwa 10 nchini, wanaotajwa na jarida la Forbe la Oktoba 2018.

Katika orodha yake, jarida hilo iliyopewa kichwa cha maneno kisemacho, “Top 10 Richest Men in Tanzania for October, 2018,” Forbe linamtaja Mohammed Dewji, kuwa ndiye anayeongoza kundi hilo. 

Wengine waliotajwa, ni pamoja na Reginald Mengi, Said Salim Bakheressa, Rostam Aziz, Shekhar Kanabar, Ally Awadh, Yusuf Manji, Subash Patel na Ghalib Said Mohammed.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Canada yatenga bilioni 38 kutekeleza mradi ya kuinua vijana TZ

Spread the loveSERIKALI ya Canada kupitia ‘CARE International Canada’ imetenga takribani Sh...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Ujenzi kituo cha kupoza umeme Chalinze wafikia asilimia 93.7

Spread the loveKamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imeeleza...

Habari Mchanganyiko

Balile ateuliwa rais wa wahariri Afrika Mashariki

Spread the loveJumuiya ya Wahariri wa Afrika Mashariki (EAES), imemchagua Mwenyekiti wa...

Habari Mchanganyiko

Jeshi la Uhifadhi kujengewa uwezo zaidi

Spread the love  WIZARA ya Maliasili na Utalii imejipanga vyema kuendelea kulijengea...

error: Content is protected !!