Baada ya kutangaza kutengana wiki chache zilizopita, bilionea Moussa Sandiana Kaba almaarufu kama Grand P kutoka Guinea amerudiana tena na mpenzi wake msanii na mlimbwende maarufu mitandaoni, Eudoxie Yao kutoka Ivory Coast. Anaripoti Mwandishi wetu. Endelea.
Mrembo Yao ambaye amebarikiwa kuwa na umbo matata namba nane, alithibitisha kutengana na mpenzi wake kupitia ukurasa wake wa facebook takriban wiki tatu zilizopita.
“Watu wangu, ni rasmi kuwa sina mchumba kwa sasa na sina nia ya kuchumbiana kwani nataka kuangazia muziki wangu. Kuweni na wikendi njema” Yao aliandika kwenye ukurasa wake wa Facebook mwishoni mwa Julai.
Hata hivyo, wiki iliyopita Grand P ambaye ni msanii na muigizaji mashuhuri nchini Guinea amepakia picha na video zao wawili ambazo zimenazoashiria kuwa wamerudiana.
Grand P alipakia picha kwenye ukurasa wake wa Instagram akiwa ameambatana na Yao na kuambatanisha na ujumbe mfupi wa mapenzi.
“Mapenzi ni kutunzana hata mkiwa mmekasirikiana. Nakupenda sana @eudoxieyao__ ” Grand P aliandika.
Kuthibitisha zaidi kuwa waliokuwa wametengana kwa sasa wako pamoja tena, kwenye mtandao wa Facebook bwanyenye huyo ambaye ana maumbile ya kipekee alipakia video mbili zilizoonyesha akiwa ameandamana na mpenzi wake Eudoxie Yao wakielekea mahali palipoonekana kuwa hoteli.
“Mguu wako, mguu wangu” Grand P aliandika chini ya video hiyo.
Mapenzi ya wasanii hao wawili yamekuwa kivutio kwa wengi kutokana na utofauti mkubwa wa kimaumbile kati yao.
Licha ya kuwa Grand P ni mtu mzima, ana mwili mdogo zaidi tofauti na watu wenye umri kama wake. Yao kwa upande wake ana mwili mkubwa kweli.
Mtu na mpenzi wake.
Mapenzi yaacheni tu. Huwezi kutafuta sababu ya wawili kupendana na ukaipata.
Kuhusu Uwekezaji kwenye Viwanja Na Majengo tembelea mtandao wa UWEKEZAJI MAJENGO.
Rafiki yenu,
Aliko Musa.
Mbobezi Kwenye Majengo.