May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Bilionea atenga mabilioni kuinunua Arsenal

Daniel Ek

Spread the love

 

PRESHA ya mashabiki wa Klabu ya Arsenal, inayoshiriki Ligi Kuu ya Uingereza kwamba timu hiyo iuzwe, imetiwa ndimu na mfanyabiashara bilionea Daniel Ek. Inaripoti mitandao ya kimataifa…(endelea).

Daniel Ek (38) ambaye ni rais wa Sweeden, Ijumaa iliyopita alitumia ukurasa wake wa twitter kueleza kile anachotaka kuifanyia Arsenal.

Mfanyabiashara huyo mwenye utajiri wa thamani ya Dola za Marekani bilioni 4.7, aliandika ‘kama mtoto niliyekulia nikiishabikia Arsenal, iwapo Kroenke (Stan Kroenke mmiliki wa klabu hiyo) yuko tayari kuiuza Arsenal, basi niko tayari kuinunua.”

Baadhi ya wachezaji wa zamani wa klabu hiyo akiwemo Thierry Henry, Dennis Bergkamp na Patrick Vieira wameungana na dhamira ya bilionea huyo anayenadi kutaka kununua klabu hiyo.

Thierry Henry

Kutokana na muendelezo wa matokea mabovu ya timu hiyo iliyoko nafasi ya 10 ikiwa na pointi 46, baada ya kucheza michezo 33, Ijumaa wiki iliyopita, mashabiki wake zaidi ya 1,000 waliandamani nje ya uwanja wa Emirate kushinikiza iuzwe.

Mpaka sasa, pamoja na presha kubwa nje ya klabu hiyo, mmilikiwa wake Kroenke ameonesha kutokuwa na mpango wa kuiuza Arsenal.

Arsenal ilikuwa imetangaza, kwamba ni miongoni mwa klabu 12 zilizojiungana na Ligi ya Ulaya ya European Superleague, Jumapili iliopita, saa 48 baadaye, walijiondoa na kuomba msamaha kwa mashabiki wake.

Alhamis iliyopita, mtoto wa Kroenke Josh, aliwaambia mashabiki wa Arsenal kwamba, familia yake haina nia ya kuuza klabu hiyo na kuahidi kujadiliana na mashabiki kuanzia sasa na siku za baadaye.

error: Content is protected !!