September 18, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Bila gesi asilia Tanzania ya viwanda ni ndoto

Spread the love

MPANGO wa Serikali ya awamu ya tano kuanzisha na kukuza uchumi wa viwanda unaweza kuwa ni ‘ndoto ya mchana’ ikiwa serikali haitajipanga katika uzalishaji wa gesi asilia na mafuta ya uhakika, anaandika Dany Tibason.

Hayo yameelezwa leo  na Francis Lupolala, afisa uhusiano wa Shirika la Maendeleo ya Petroli hapa nchini (TPDC), alipokuwa akitoa maelezo katika mafunzo ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari kutoka mikoa wa Dodoma na Singida kwa lengo la kuitambua vyema TPDC na kazi zake.

“Sera ya Taifa ya Tanzania kuwa nchi ya viwanda haiwezi kutimia ikiwa hakuna gesi asilia ya kutosha pamoja na mafuta ya uhakika, TPDC inafanya kazi vizuri ili wananchi wajue wananufaikaje na rasilimali inayopatikana katika nchi yao,” amesema.

Christina Mdeme, Mkuu wa Wilaya ya Dodoma amewataka waandishi kutumia kalamu zao kiuzalendo kwa kuitangaza vyema nchi yao ikiwa ni pamoja maliasili zilizopo nchini ili kuwafanya wageni kuvutiwa na kuwafanya washawishike kuwekeza.

“Tunaelekea katika nchi ya uchumi wa kati wa viwanda, tunahitaji kuwa na gesi ya kutosha, umeme na mafuta hivyo wanahabari mkitumia vyema kalamu zenu kwa uzalendo tutapata wawekezaji kwa ajili ya kujenga viwanda au kuchimba gesi ya kutosha,” amesema.

DC huyo amesisitiza kuwa, iwapo kalamu za waandishi wa habari zitatumika vibaya bila kuzingatia uzalendo, zinaweza kuisababishia hasara nchi ikiwemo kuijengea taswira mbaya mbele ya wageni.

error: Content is protected !!