Wednesday , 24 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Bil 68 tozo ya miamala ya simu, mafuta zakusanywa, punguzo bado
Habari za SiasaTangulizi

Bil 68 tozo ya miamala ya simu, mafuta zakusanywa, punguzo bado

Spread the love

 

SERIKALI ya Tanzania, imekusanya zaidi ya Sh.68 bilioni, kupitia tozo ya miamala ya simu na mafuta. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Hayo yameelezwa leo Ijumaa, tarehe 29 Agosti 2021 na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Mwigulu Nchemba, wakati akitoa kauli ya Serikali juu ya hatua ambayo imefikia kuhusu marekebisho ya tozo ya miamala ya simu, jijini Dar es Salaam.

Amesema kati ya fedha hizo, zilizokusanywa kupitia tozo ya miamala ya simu iliyoanza tarehe 15 Julai 2021, ni Sh. 48.4 bilioni. Huki Sh. 20 bilioni ikitoka katika tozo ya mafuta.

“Licha ya kwamba Serikali inafanyia kazi mapendekezo ya wananchi, hii ilikuwa Sheria ya Bunge, tuliendelea kutumia kwa wakati tukifanyia kazi. Shughuli hii imeanza tarehe 15 Julai, mpaka leo ukioanisha na mapendekezo tuliyokuwa tumepangilia, tayari tumekusanya Sh. 48.48 bilioni,” amesema Dk. Mwigulu.

Dk. Mwigulu amesema, Serikali imepeleka Sh. 22 bilioni, katika Wizara Ofisi ya Rais-Tamisemi, kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya afya.

Pia, Dk. Mwigulu amesema Serikali imekusanya zaidi ya Sh. 20 bilioni, kupitia tozo ya mafuta, iliypqnza kutozwa tarehe 1 Julai mwaka huu.

“Upande wa tozo ya mafuta mwezi ulipita wa Julai, ambayo na yenyewe mpaka wiki ijayo Tamsiemi watakuwa wamepokea Sh. 24 bilioni, hizo ni mahusi kwa ajili ya barabara za vijijini. Kutoka tarehe 1 Agosti 2021, tutakuwa na zaidi ya Sh. 20 bilioni nyingine na kuendelea,” amesema Dk. Mwigulu.

“Tunakubaliana kama nchi kwamba tuna miradi ambayo inaendelea na lazima iendelee kutekelezwe, lakini kuna masuala ambayo yanahitaji uangalizi wa haraka.”

Dk. Mwigulu Nchemba, Waziri wa Fedha na Mipango

“Tumeona ni vema kuhabarisha umma kuhusu tozo, ombi langu moja ni hili jambo ni letu sote, si la serikali. Kila mtanzania ulipo, lazima utambue nchi ni yako na pesa ni yako hapo ulipo na haya tunataka kufanya ni yako, sisi tunaofanya ni dhamana tu,” amesema.

Waziri huyo amesema, “leo kutakuwa na kikao cha kupokea taarifa, kwa hiyo si muda mrefu tutatoa tamko la mwisho kuhusu namba hizo kwa hiyo Watanzania wamekuwa wavumilivu tunawoamba waendelee wawe na subira.”

Kuhusu kupungua kwa miamala baada ya tozo kuanza, Dk. Mwigulu amesema “hapa katikati kuliibuka maneno mengi sana na ilielezwa shughuli za miala ilipungua, niseme kwamba Watanzania waliendelea kutumiana na shughuli za kufanya miamala hazikuathirika na takwimu ziko pale pale.”

Ummy Mwalimu

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais- Tamisemi, Ummy Mwalimu, amesema wizara hiyo imepokea Sh. 22. 5 bilioni kwa ajili ya kujenga vituo vya afya katika Halmashauri 82 za Tanzania Bara.

“Wizara imepokea kutoka hazina Sh. 22.5 bilioni, kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya afya 90. Vitajengwa katika halmashauri 82 za Tanzania Bara . Tuna 184 halmashauri, kwa hiyo 82 wanufaika na pesa hizo na zimefika halamshauri husika,” amesema Ummy.

2 Comments

  • Tunataka kuona hivyo vituo vya afya vikikamilika la sivyo fedha hizo zitaliwa na wajanja. Tusubiri ripoti ya CAG. Nasema uwongo ndugu zangu?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

Habari za Siasa

Serikali kuanzisha mradi wa Gridi ya maji ya Taifa

Spread the loveWaziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema katika mwaka wa fedha...

error: Content is protected !!