Wednesday , 24 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Bil 600 tozo ya simu kutumika hivi
Habari MchanganyikoTangulizi

Bil 600 tozo ya simu kutumika hivi

Spread the love

 

SERIKALI ya Tanzania, imesema zaidi ya Sh. 600 bilioni, zitakazotokana na kodi mpya ya mitandao ya simu, zitatumika katika utekelezaji miradi ya elimu, afya ya msingi na miundombinu ya barabara. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Taarifa hiyo imetolewa jana Jumanne, tarehe 6 Julai 2021 na Waziri Ofisi ya Rais-Tamisemi, Ummy Mwalimu, akizungumza na wanahabari jijini Dodoma.

Waziri huyo amesema, Sh.125 bilioni zitaenda kuboresha sekta ya elimu, kwa kukamilisha ujenzi wa vyumba vya madarasa 10,806 vya shule za msingi na sekondari na mabweni ya shule za sekondari za sayansi za wasichana.

“Katika ile kodi ya mitandao ya simu, Tamisemi tumepata Sh.125 bilioni, kwenye hizi hela tunaenda kukamilisha ujenzi wa vyumba vya madarasa 10,000. Vyumba 7,499 ni vya madarasa ya shule za msingi na 2,501, kwa ajili ya sekondari,” amesema Ummy.

Ummy amesema “tunakwenda kujenga maabara za sayansi 1,043, kujenga shule za sekondari za kata 300 na tunakwenda kujenga shule za sekondari za sayansi za wasichana 10.”

Kwenye sekta ya afya, Ummy amesema, Tamisemi imepewa Sh. 200 bilioni, ambazo zitatumika kujenga na kukamilisha zahanati 756, zinazogharimu Sh. 38.15 bilioni, ukamilishaji ujenzi wa maboma 900 ya zahanati (Sh. 45 bilioni). Na Sh. 112 bilioni zitatumika kununua vifaa tiba.

“Kupitia fedha hizo, kila jimbo litapata wastani wa zahanati tatu, vijiji 900 vitapata zahanati moja moja. Sh. 112 bilioni zitanunua vifaa tiba. Pia kupitia fedha hizo, Sh. 55 bilioni zitakamilisha ujenzi vituo vya afya 114, vilivyojengwa kwa zaidi ya miaka 10,”amesema Ummy.

Kwa upande wa miundombinu, Ummy amesema Sh. 322 bilioni zitatumika kujenga barabara za kiwango cha lami zenye urefu wa kilomita 250, kupandisha hadhi barabara za changarawe kuwa mawe, zaidi ya kilomita 5,834 na madaraja makubwa 64.

Kwa mujibu wa tozo hizo mpya, Sh. 10 hadi 10,000, zitatozwa katika kila muamala wa kutuma au kutoa pesa kulingana na thamani ya muamala wa fedha husika.

Pia, Sh. 10 hadi 200 zitatozwa kwa kila laini kulingana na matumizi ya mmiliki.

Tozo hizo zimeanza kutumika Julai Mosi 2021, baada ya Serikali kuanza utekelezaji wa bajeti yake kwa mwaka wa fedha wa 2021/2022.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

THRDC yaongeza mkataba wa ushirikiano na ABA

Spread the love  MTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC),...

Habari Mchanganyiko

Rufaa ya Equity Benki, State Oil yakwama

Spread the loveMAHAKAMA ya Rufani, jijini Dar es Salaam, imeshindwa kuendelea na...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari Mchanganyiko

Bodaboda waeleza mafanikio mafunzo usalama barabarani

Spread the loveMADEREVA bodaboda katika Jiji la Dodoma wameeleza jinsi mafunzo ya...

error: Content is protected !!