January 25, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Bil 500 zahitajika kusambaza dawa nchi nzima

Spread the love

BOHARI Kuu ya Dawa nchini (MSD) imedai kuwa licha ya Serikali kuilalamikia kwamba hushindwa kupeleka dawa za kutosha katika vituo vya afya na hospitali za wilaya na mikoa, imedai kikwazo kinachosababisha kukosekana kwa dawa ni bajeti ndogo. Anaandika Moses Mseti, Mwanza … (endelea).

Kauli hiyo imetolewa leo na Mkurugenzi Mtendaji wa MSD, Laurean Bwanakunu, wakati wa uzinduzi wa Duka dawa la jumla na rejareja, uliofanyika katika hospitali ya mkoa wa Mwanza Sekou Toure, mjini hapa.

Amesema ili vituo vya afya na hospitali ziweze kupata dawa na kufanya kazi yake kwa ufanisi na dawa za kutosha ziweze kupatikana kwenye hospitali hizo za Serikali inahitajika Sh. 577 bilioni.

Bwanakunu amesema kuwa Serikali imekuwa ikiilalamikia MSD kwamba imekuwa ikishindwa kusambaza dawa katika hospitali za Serikali huku ikishindwa kutambua tatizo bajeti inayotengwa.

“Sasa hivi vituo vya afya na hospitali za Serikali zinapokea bajeti ya Sh. 80 bilioni lakini kiasi hicho hakitoshi kabisa na ili huduma itolewe ya uhakika na dawa ziweze kupatikana inatakiwa Sh. 577 bilioni.

“Rais (Dk. John Magufuli) ameahidi kuongeza bajeti katika wizara ya afya kufikia kiasi cha Sh. 577 bilioni, tunatarajia sasa kiasi hicho kitaweza kupunguza ama sio kumaliza kabisa tatizo la dawa hospitalini,” amesema Bwanakunu.

Hata hivyo amesema licha ya ukusanyaji wa mapato kuwa mkubwa katika hospitali za mikoa na vituo vya afya nchini lakini kiasi cha bajeti kinachotengwa hakilingani na ukusanyaji huo wa mapato.

Pia amesema kufunguliwa kwa duka hilo kubwa katika mkoa wa Mwanza, litaweza kuhudumia hospitali za mikoa ya kanda ya ziwa na kuweza kupunguza tatizo la ukosefu wa dawa hospitalini.

Meneja wa MSD kanda ya ziwa, Byekwaso Tabura, amesema duka hilo limeghalimu kiasi cha Sh. 27 milioni na litakuwa linauza dawa za kila aina na ambazo zilikuwa hazipatikani hospitalini.

error: Content is protected !!