January 19, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Bil 500 kujenga nyumba za polisi

Spread the love

SERIKALI inakamilisha taratibu za kukopa kiasi cha Sh. 500 bilioni kutoka Benki ya Xim ya nchini China kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za polisi. Anaandika Dany Tibason … (endelea).

Kauli hiyo imetolewa leo Bungeni na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hammed Yusufu Masaun alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Momba, David Silinde (Chadema).

Mbunge huyo alitaka kujua serikali ina mpango gani wa kuhakikisha nyumba za askari zinajengwa ili kuwaondoa katika adha kubwa ya kuishi kwenye nyumba ambazo hazina hadhi.

Mbali na hilo alitaka kuelezwa ni kwanini Kitengo cha Usalama Barabarani wasitumie makusanyo yao ya fedha zinazotokana na faini za makosa mbalimbali ya magari kutumika kujenga nyumba za askari hao.

Pia Mbunge wa Konde, Khatibu Haji Kombo (CUF) katika swali la nyongeza alitaka serikali imueleze ni lini askari wa Konde wataachana na adha ya kulala katika magofu.

Pia alitaka kujua kama mpango wa ujenzi wa nyumba za askari unahusisha na Jimbo la Konde na ni nyumba ngapi zitajengwa.

Awali katika maswali ya msingi ya Mbunge wa Tunduma, Franka Mwakajoka (Chadema) alitaka kujua serikali ina mpango gani wa kujenga Kituo cha Polisi chenye hadhi ya Wilaya ya Tumduma ili kuendana na ongezeko la watu na wageni wanaoingia nchini.

Pia alitaka kujua kama serikali haioni kuwa ni vyema ujenzi wa kituo hicho uendane sambamba na ujenzi wa nyumba zenye gharama nafuu kwa polisi ambao wanashida kubwa ya makazi.

Akijibu maswali hayo Masauni amesema serikali inakusudia kujenga nyumba 35,000 kila mwaka hadi ifikapo mwaka 2025.

Aidha amesema fedha zote ambazo hukusanywa na Jeshi la Polisi Kitengo cha Usalama Barabarani hupelekwa Hazina na si vinginevyo.

Kuhusu ujenzi wa nyumba za askari amesema kwa sasa serikali imeingia katika makubaliano ya kukopa kiasi cha Sh. 500 Bilioni 500 kutoka Benki ya Xim ya China kujenga nyumba za askari huku nyumba 150 zikitarajiwa kujengwa Konde.

Amesema, kwa sasa serikali inakamilisha taratibu za kupata mkopo huo kwa ajili ya ujenzi wa nyumba 4,136 za makazi ya askari katika mikoa 17 nchini.

Amesema Kituo cha Polisi cha Tunduma ni kidogo na hakina nyumba za kutosha kwa ajili ya askari hivyo Wilaya ya Momba inahitaji 150 ili kukidhi mahitaji ya makazi ya askari.

error: Content is protected !!