Thursday , 18 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Bil. 33 kutumika kuimarisha huduma za kijamii nchini
Habari za Siasa

Bil. 33 kutumika kuimarisha huduma za kijamii nchini

Waziri wa Nchi Ofisi a Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), Ummy Mwalimu
Spread the love

WIZARA ya Afya, kupitia Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii inatarajia kutumia Jumla ya Sh. 33.1 bilioni kutekeleza shughuli mbalimbali za kijamii hususani zilizopewa kipaumbele kwa mwaka wa fedha 2020/21. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Akiwasilisha Hotuba ya Wizara, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema katika mwaka wa fedha 2020/21 Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii inatarajia kutumia kiasi hicho cha fedha kwa lengo la kuimarisha huduma na mafunzo kwenye Taasisi za Ustawi na Maendeleo ya Jamii, kukarabati makazi ya wazee, kujenga mahubusu za watoto na kutokomeza ukatili wa kijinsia.

Amesema kuwa bajeti hiyo itasaidia kuimarisha kujenga kumbi pacha na hosteli katika Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru ambapo jumla ya Sh. 2.7 bilioni zimetengwa, pia kuboresha utoaji wa mafunzo ya taaluma ya maendeleo ya jamii ili kukidhi mahitaji ya soko sambamba na kukuza ujuzi wa wahitimu ikiwemo kuwajengea uwezo wa kujiajiri na kuajiriwa kwa kutenga jumla ya Sh. 6.6  bilioni.

Maeneo mengine yaliyotengewa fedha ni pamoja na ukarabati wa majengo na miundombinu katika makazi ya wazee kwa Sh. 400 milioni, ujenzi wa Shule ya Maadilisho katika Mkoa wa Geita Sh. 200 milioni, kuimarisha ujenzi wa mahabusu ya watoto katika mikoa ya Kigoma na Mtwara Sh. 700 milioni na kuwezesha Taasisi ya Ustawi wa Jamii kuboresha utoaji wa mafunzo yanayokidhi mahitaji ya soko Sh. 250 milioni.

Aidha, jumla ya Sh. 826.95 milioni zimetengwa kwa ajili ya shughuli za kutokomeza ukatili wa kijinsia katika jamii.

“Ili kutekeleza vipaumbele vilivyoanishwa kwa mwaka 2020/21, Wizara kupitia Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii imekadiria kutumia kiasi cha Sh. 33 bilioni kwa ajili ya kutekeleza majukumu mbalimbali ya Wizara ikiwa ni pamoja na uendeshaji wa ofisi na miradi ya maendeleo,” amesema Ummy.

Ummy amesema Wizara imeendelea kukuza ari ya jamii kushiriki katika kujiletea maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwa kutumia nguvu kazi na rasilimali zinazowazunguka na kusimamia masuala yote ya ushirikishwaji wa jamii kwenye sekta mbalimbali.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

Habari za Siasa

CCM yamkana mwenyekiti UVCCM aliyetaka wapinzani wapotezwe

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimejitenga na kauli ya mwenyekiti...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia kutunukiwa udaktari wa heshima Uturuki

Spread the loveBaraza la Chuo Kikuu cha Ankara, ambacho ni cha pili...

error: Content is protected !!