Thursday , 30 March 2023
Home Kitengo Maisha Afya Bil 14 kujenga hospitali 28
AfyaHabari za Siasa

Bil 14 kujenga hospitali 28

Ummy Mwalimu, Waziri wa TAMISEMI,
Spread the love

 

SERIKALI imetenga Sh. 14 Bilioni kwa ajili ya kuanza ujenzi wa hospitali mpya 28, ikiwepo Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga iliyotengewa sh.500 Milioni. Anaripoti Jemima Samweli, DMC … (endelea).

Kauli hiyo imetolewa leo Tarehe 20 April 2021, bungeni jijini Dodoma na Ummy Mwalimu, Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi).

Ummy ametoa kauli hiyo baada ya Jonas Mbinga, Mbunge Mbinga Vijijini kuiomba serikali ieleze, lini itaanza kujenga na kukarabati majengo ya Hospitali ya Wilaya ya Mbinga kutokana na kukosa baadhi ya majengo kwani yaliyopo, yamechakaa.

“Serikali inatambua uchakavu wa baadhi ya hospitali kongwe za halmashauri ikiwemo Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga.

“Kwa kuzingatia hali hiyo, serikali imeona ni vema katika mwaka wa fedha 2021/22 kutenga na kuomba kuidhinisha Sh.14 Bilioni kwa ajili ya kuanza ujenzi wa mpya wa hospitali 28, ikiwemo Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga iliyotengewa Sh.500 Milioni,” amesema.

Waziri huyo pia amesema, serikali imeendelea kutenga fedha kwa ajili ya kuboresha huduma za afya kwa kukarabati na kujenga hospitali mpya nchini, kwa awamu kadri ya upatikanaji wa fedha,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

TEMESA iliyokarabati Kivuko kwa Bil 7.5 yapata hati chafu

Spread the love  MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),...

Habari za Siasa

ACT-Wazalendo yakusanya Mil 8.5/- kodi ya zuio na kutokomea nazo

Spread the love  MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),...

Habari za Siasa

DC Kasilda Mgeni ahamasisha chakula shuleni

Spread the love  MKUU wa Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro, Kasilda Mgeni...

Habari za Siasa

Bilioni 223.9 zapelekwa Tunduru ndani ya miaka 2 ya SSH

Spread the love  ZAIDI ya Sh. bilioni 223.9 zimepelekwa Wilaya ya Tunduru...

error: Content is protected !!