January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Bil. 105/- kupanua uwanja Mwanza

Uwanja wa Ndege wa Mwanza

Spread the love

JUMLA ya Sh. 105 bilioni zimekadiriwa kutumika katika mradi wa upanuzi wa kiwanja cha ndege cha Mwanza. Anaandika Dany Tibason … (endelea).

Kauli hiyo imetolewa leo bungeni na Waziri wa Uchukuzi, Samuel Sitta alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Maria Hewa (CCM), aliyetaka kujua ni lini ukarabati wa uwanja na majengo yake utafanyika.

Akijibu swali hilo, Sitta amesema serikali inaendelea kufanya juhudi za upatikanaji wa fedha kwa lengo la kukamilisha mradi huo kwa wakati ili kukidhi malengo yaliyokusudiwa. 

Ametaja kazi zinazoendelea kupitia Mkandarasi Kampuni ya Beijing Construction Engineering Group Company Ltd kuwa ni ujenzi wa jengo jipya la abiria pamoja na miundombinu yake, ujenzi wa jengo la kuongozea ndege na jengo la kuhudumia mizigo.

Nyingine ni urefushwaji wa njia ya kuruka au kutua ndege, maegesho ya ndege za mizigo na viungio vyake, kuhamisha mto na mfumo wa maji safi na taka na kituo cha umeme.

Kwa mujibu wa Sitta, baada ya kukamilika kwa ukarabati na upanuzi wa kiwanja pamoja na ujenzi wa jengo la abiria na mizigo, kiwanja kitakuwa na uwezo wa kuhudumia abiria milioni mbili kwa mwaka.

“Hivyo, majengo yote yanayotumika kwa sasa yatabomolewa ili kupisha eneo hilo kuwa salama,” amesema.

error: Content is protected !!