August 10, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Bil 1.6 kujenga madawati Kinondoni

Spread the love

 

HALMASHAURIya Manispaa ya Kinondoni imetia saini mikataba yenye thamani ya Sh. 1.6 bilioni kwa ajili ya kutengeneza madawati katika Shule za Misingi na Sekondari kwenye manispaa hiyo, anaandika Pendo Omary.

Mikataba hiyo imetiwa saini na Boniface Jacob, Meya wa Manispaa ya Kinondoni kwa niaba ya manispaa hiyo na wakandarasi tisa ambapo wanatakiwa kukabidhi madawati hayo mwezi Julai mwaka huu.

Akizungumza wakati wa shughuli hiyo, Jacob amesema “mikataba hii yenye thamani ya Sh. 1.6 bilioni itawezesha kutengeneza madawati 12,091 kwa shule za msingi, viti 6,552 na meza 6,552 kwa shule za sekondari. Mpaka kufikia 30 Agosti hakuna mwanafunzi atakae kaa chini.

“Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni ameamua kutoa zabuni kwa wakandarasi tisa ili kuwezesha kazi hiyo kukamilika kwa wakati na kwa ubora utakaolingana na thamani ya fedha itakayotumika (value for money),” amesema Jacob.

Aidha, Jacob amesema fedha hizo ni sehemu ya Sh. 1.8 bilioni fedha ambazo zimetokana na kusimamisha posho za siku tangu mwezi Aprili kwa nafasi za meya, mkurungezi wa manispaa, wahandisi, ofisa watumishi na wanasheria bila kugusa posho za madaktrai, manesi na madiwani.

Kampuni zilizopewa zabuni hiyo ni Msikale itakayotengeneza madawati 500 ya shule za msingi, meza 500 na viti 500 vya shule za sekondari kwa gharama ya Sh. 87,500,00. Mtweve Worksho itatengeneza madawati 1000 kwa shule za msingi, viti 500 na meza 500 kwa shule za sekondari kwa gharama ya Sh. 132,500,500.

“Pia Highland Traders and General Services watatengeneza madawati 500 ya shule za msingi, meza 500 na viti 500 kwa shule za sekondari yenye thamani ya Tsh. 87,500,000. Mai Hardware Supplies atakaetengeneza madawati 500 kwa shule za msingi na meza 500 kwa shule za sekondari kwa Sh. 87,500,500,” amesema Jacob.

Jacob ametaja wazabuni wengine kuwa ni Edosama Hardware ambayo itatengeneza madawati 5091 kwa shule za msingi, viti 2052 na meza 2052 kwa shule za sekondari kwa Sh. 662,610,000, Kampuni ya Unipro Solution itatengeneza madawati 2000 kwa shule za msingi, viti 500 na meza 500 kwa shule za sekondari kwa Sh. 222,500,500.

Wengine ni Bwanza Investment Company itatengeneza madawati 500 kwa shule za msingi, viti 500 na meza 500 kwa shule za sekondari kwa Sh. 87,500,500, Benema Enterprises itatengeneza madawati 500 kwa shule za msingi, viti 500 na meza 500 kwa shule za sekondari kwa Sh. 87,500,500.

“Na mwingine ni Mazongera Furniture and Decoration Supply, kampuni hii itakaetengeneza madawati 1500 kwa shule za msingi, viti 100 na meza 1000 kwa shule za sekondari kwa Sh. 220,000,000,” amesema Jacob.

 

error: Content is protected !!