Thursday , 28 March 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Biden, Xi wasisitiza haja ya kupunguza migogoro
Kimataifa

Biden, Xi wasisitiza haja ya kupunguza migogoro

Spread the love

 

VIONGOZI wa Marekani na China wamekutana katika hatua ambayo inalenga kutuliza joto la mzozo kati ya nchi zao. Anaripoti Mwandishi Wetu kwa msaada wa mashirika ya kimataifa.

Katika hotuba yake ya ufunguzi, Rais wa Marekani Joe Biden alizungumzia umuhimu wa kuepuka “migogoro” kati ya Marekani na China.

Biden alisema “amejitolea kuweka njia ya mawasiliano kati yetu wazi” ili nchi hizo mbili “zifanye kazi pamoja katika masuala ya dharura ya kimataifa” ikiwa ni pamoja na mabadiliko ya hali ya hewa na ukosefu wa usalama.

Ulimwengu “unatarajia” mataifa hayo mawili kufanya kazi kwa ushirikiano, Biden aliongeza.

Kwa mujibu wa BBC kile ambacho Beijing inataka katika mkutano huo na kile inachotarajia kufikia ni mambo mawili tofauti.

Serikali zote mbili za China na Marekani hazidanganyiki kuhusu jinsi mvutano ulivyo mkubwa kati ya mataifa yenye nguvu kubwa duniani na hazitategemea mafanikio fulani ya miujiza ili kurudisha mahusiano kama yalivyokuwa zaidi ya muongo mmoja uliopita.

Kwa mfano, wakati Washington inaishutumu China kwa mazoea ya biashara ya kutumia nguvu, utawala wa Xi Jinping ungeelekeza vikwazo muhimu vya Marekani kwa sekta ya teknolojia inayoibukia ya China.

Hata hivyo itakuwa jambo la kushangaza kwa waangalizi wengi ikiwa mojawapo ya vikwazo hivi vitaondolewa kufuatia mkutano huu.

Hakuna upande unaotaka hesabu potofu kuhusu tabia ya mwingine kusababisha vita. Marekani inazungumza kuhusu “vituo vya ulinzi” kuwekwa. Hii inaweza kuhusisha njia wazi za mawasiliano na hata seti ya sheria au labda mistari ya rangi nyekundu isiyopaswa kuvukwa.

Taiwan ndio kielekezi kinachowezekana lakini sio pekee. Vita vya Ukraine na majaribio ya makombora ya Korea Kaskazini pia yameongeza mvutano kati ya Beijing-Washington. Yote haya yanaweza kujadiliwa vizuri.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifa

Mwanaye rais jela miaka miaka 6 kwa dawa za kulevya

Spread the loveMwanawe rais wa zamani wa Guinea-Bissau amehukumiwa kifungo cha miaka...

Habari za SiasaKimataifa

Faye aahidi kuongoza kwa unyenyekevu, wagombea wenzie wakubali yaishe

Spread the loveMgombea wa upinzani Senegal, Bassirou Diomaye Faye anajiandaa kuwa rais...

Habari MchanganyikoKimataifa

Wanafunzi 130 waliokuwa wametekwa nyara waokolewa

Spread the loveZaidi ya wanafunzi 130 wa shule ya msingi LEA na...

Habari MchanganyikoKimataifa

Mgombea upinzani aongoza uchaguzi wa Rais Senegal

Spread the loveMgombea wa upinzani nchini Senegal, Bassirou Diomaye Faye ameonekana kuongoza...

error: Content is protected !!