October 2, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Biden aimwagia Ukraine matrilioni kuendelea na vita

Spread the love

 

RAIS wa Marekani, Joe Biden ametia saini mkataba wa kutoa fedha kiasi cha Dola za Marekani milioni 600 (sawa na Sh trilioni 1.3) ikiwa ni msaada wa haraka wa kijeshi kwa taifa la Ukraine. Inaripoti Mitandao ya kimataifa … (endelea).

Agizo hilo linamuelekeza Waziri wa Mambo ya Nje ya Marekani, Antony Blinken kutoa msaada wa kijeshi wa haraka kwa Ukraine wa hadi dola za Marekani milioni 250 ili kulisaidia taifa hilo bila kuzingatia kifungu chochote cha sheria.

Awali zaidi ya dola za Marekani milioni 350 zaidi zilitengwa kwa ajili ya kutoa huduma za ulinzi na mafunzo ya kijeshi.

Biden alitoa pesa hizo jana tarehe 25 Februari, 2022 huku Rais wa Ukraine, Volodymr Zelensky akifichua kuwa alipuuza pendekezo la Marekani la kumtaka kuuhama mji mkuu wa Kyiv.

Rais wa Marekani, Joe Biden

Marekani ilimpa ofa hiyo Rais huyo wa Ukraine baada ya kupata taarifa kuwa Rais wa Urusi, Vladimir Putin ametuma vikosi vya utekaji nyara kumteka nyara au kumuua.

Zelensky alisema; Mapambano yapo hapa. Nahitaji risasi, si kupanda ndege na kukimbia.”

Kauli hiyo ya Zelensky imekuja saa chache kabla ya wanajeshi wa Urusi kudaiwa kuanza kuuzunguka mji wa Kyv wakati mapambano yakizidi kusika kasi kwa siku ya tatu sasa.

error: Content is protected !!