Wednesday , 29 March 2023
Home Kitengo Habari Kimataifa Biden afanya ziara ya kushtukiza Ukraine
Kimataifa

Biden afanya ziara ya kushtukiza Ukraine

Spread the love

RAIS wa Marekani Joe Biden amewasili Kyiv – ziara yake ya kwanza nchini Ukraine tangu Urusi ilipovamia karibu mwaka mmoja uliopita. Imeripoti Mitandao ya habari ya kimataifa…(endelea)

Ziara hiyo ya kushtukiza imekuja wakati alipokuwa akisafiri kwenda nchi jirani ya Poland kukutana na Rais Andrzej Duda.

Dakika chache Rais wa Ukraine Zelensky ameshirikisha picha kwenye akaunti yake rasmi ya Telegram akipeana mkono na rais wa Marekani.

Kulikuwa na uvumi mapema leo Jumatatu tarehe 20 Februari 2023 kwamba mgeni muhimu alikuwa akiwasili katika mji mkuu wa Ukraine, ambao mwanasiasa wa Ukraine Lesia Vasylenko amethibitisha kuwa ni Biden.


Safari ya siri ya Biden kwenda Ukraine ilifanywa kupitia treni kutoka mpaka wa Poland, gazeti la New York Times linaripoti.

Ziara ya Kyiv ilifanywa kisiri kwa sababu ya tahadhari ya kiusalama.

Ripoti pia zinasema kwamba Biden aliondoka Washington bila taarifa baada ya yeye na mkewe Jill kula chakula cha jioni kwenye mkahawa Jumamosi usiku.

Maafisa walikuwa wamekanusha kuwa Biden angezuru Ukraine wakati wa safari yake ya kuelekea Ulaya mashariki.

Gazeti la The New York Times linasema: “Hakika, Ikulu ya Marekani Jumapili usiku ilitoa ratiba ya hadharani Jumatatu ikimuonyesha rais bado yuko Washington na kuondoka jioni kuelekea Warsaw, wakati alikuwa tayari ameanza safari.”

Kabla ya mkutano na waandishi wa habari, Joe Biden alifanya mazungumzo na Volodymyr Zelensky na kusema kwamba “anatazamia kujadili ulimwengu” pamoja naye.

Pia aliwasifu raia wa Ukraine kwa mapigano yao ya “kishujaa” – licha ya ukosefu wa uzoefu wa kijeshi. Alisema: “Tena cha kustaajabisha ni kwamba watu wa Ukraine ni raia wa kawaida, wachapakazi, ambao hawakuwahi kupata mafunzo ya kijeshi, lakini jinsi walivyopiga hatua ya kishujaa ni jambo ambalo na ulimwengu wote unajivunia.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Nyumba ya babu yake Makamu wa Rais wa Marekani yatafutwa Zambia

Spread the love  KAMALA Harris, makamu wa rais wa Marekani, amepanga kutembelea...

Kimataifa

Benki ya Uswizi mbioni kuziwekea vikwazo akaunti za siri za Wachina

Spread the love  WAKATI Serikali na Benki ya Uswizi ikichukua hatua kali...

Kimataifa

Netanyau asitisha mipango yenye utata marekebisho mfumo wa sheria

Spread the love  WAZIRI Mkuu wa nchini Israel, Benjamin Netanyahu amesema atachelewesha...

Kimataifa

Raila ahutubia waandamanaji, mabomu yarindima

Spread the loveMSAFARA wa kiongozi wa Azimio la Umoja-One Kenya, Raila Odinga...

error: Content is protected !!