Saturday , 25 March 2023
Home Kitengo Habari Kimataifa Biden aanza kuzika sera za Trump 
KimataifaTangulizi

Biden aanza kuzika sera za Trump 

Joe Biden, Rais wa Marekani
Spread the love

HATA kabla ya saa 24 kupita tangu kuapishwa kwake kuwa Rais wa 46 wa Marekani, Joe Biden tayari amebatilisha baadhi ya sera za mtangulizi wake Donald Trump. Inaripoti mitandao ya kimataifa…(endelea).

Biden amebadili utaratibu wa kupamana na virusi vya corona (COVID-19), kwamba kutakuwa na uvaaji wa barakoa katika maeneo yote ya umma na wakati wote.

Amesema, anairejesha Marekani katika Shirika la Afya (WHO) ambapo Trump aliliondoa taifa hilo.

Biden ameondoa mkakati wa kugharamia ujenzi wa ukuta kati yake na Taifa la Mexico, Trump alipoingia madarakani katika kukabiliana na kile alichoita wahamiaji harama, aliweka mpango wa ujenzi wa ukuta huo.

Donald Trump

Lakini pia, rais huyo mpya amepuuza na kutokomeza sera ya Trump ya kuzia watu wanaotoka katika mataifa ya Kiislamu kuingia Marekani.

Ujenzi wa bomba kupitisha mali ghafu kutoka Alberta, nchini Canada mpaka Nebraska lililokadiriwa kugharimu Dola za Marekani bilioni 8, lililoidhinishwa na Barack Obama (2015), lilipigwa marufuku na Trump lakini ujenzi huo uneahidiwa kurejea kwenye mazungumzo ya kuuendeleza.

Biden ameapishwa jana tarehe 20 Januari 2021, upaishwaji wake umehudhuriwa na watu wachache pia na marais wastaafu wa taifa hilo Obama ambaye Biden alikuwa makamu wake wa rais kwa miaka minane, Bill Clinton na George W Bush.

Pia aliyekuwa makamu wa rais wa Trump, Mike Pence. Hata hivyo, Trump aligoma kuhudhuria hafla hiyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Mpinzani mkuu wa Rais Kagame aachiwa huru

Spread the love  PAUL Rusesabagina, aliyewahi kuripotiwa kama ‘shujaa’ katika filamu ya...

Kimataifa

Rais Tshisekedi amteua kiongozi wa wanamgambo kuwa Waziri wa Ulinzi

Spread the love  RAIS wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Felix Tshisekedi,...

Kimataifa

Raila Odinga: Tutafanya maandamano makubwa mara mbili kwa wiki

Spread the love KIONGOZI wa upinzani nchini Kenya, Raila Amollo Odinga ametangaza...

Kimataifa

Magharibi kuwekeza silaha Indo-Pacific, China yachochea

Spread the love KUVUNJIKA ushirhikiano wa China na Magharibi uliodumu kwa takribani...

error: Content is protected !!