KIONGOZI wa Chama cha upinzani nchini Uganda cha National Unity Party (NUP), Robert Kyagulanyi maarufu Bobi Wine amesema, atakwenda mahakamani kupinga matokeo yaliyompa ushindi wa urais Yoweri Mseven. Inaripoti mitandao ya kimataifa … (endelea).
Bobi Wine alikuwa miongoni mwa wagombea urais katika uchaguzi mkuu uliofanyika tarehe 14 Januari 2021 ambapo, Tume ya Uchaguzi Uganda (EC), ilimtangaza Museveni kuwa mshindi kwa kupata kura 5,851,037 sawa na asilimia 58.64 ya kura zote zilizopigwa.
Bobi Wine, alishika nafasi ya pili akipata kura 3,475,398 sawa na asilimia 34.83 ya kura zote 9,978,093 ikiwa ni sawa na asilimia 57.22 ya idadi ya watu waliojiandikisha kwenye daftari la wapiga kura.

Kutokana na matokeo hayo, chama cha NUP kimetoa taarifa ya kwenda kupinga matokeo hayo mahakamani huku kikiwataka wanachama wao, kutokufanya fujo.
Bobi Wine alitumia ukurasa wa Twitter wa NUP kutoa ujumbe kwa wafuasi wake akisema “nachukua uamuzi huu kwa uchungu kuwasihi kujizuia kufanya aina yoyote ya fuju. Tunajiandaa kuwasilisha mahakamani malalamiko ya kupinga matokeo ya uchaguzi yaliyokuwa na kasoro za dhahiri kwa maslahi ya ushindi wa muda mrefu ujao na kwa Uganda.”
Leave a comment