July 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Biashara United kupanda ndege kimataifa mwakani

Spread the love

 

KLABU ya Biashara United, kutoka Mara imefanikiwa kushiriki michuano ya kimataifa kwa msimu ujao, mara baada ya kumaliza katika nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Kwa sasa Biashara United ina pointi 50, kufuatia kupata matokeo ya sare ya bao 1-1, kwenye mchezo wa jana dhidi ya Tanzania Prisons, pointi ambazo hazotaweka kufikiwa na KMC ambao wapo kwenye nafasi ya tano wakiwa na alama 45, huku ukisalia mchezo mmoja.

Biashara United inashikili michuano hiyo, kufuatia Tanzania kupata ushiriki wa timu nne kwenye msimu ujao wa mashindano ya kimataifa.

Klabu hiyo inakamilisha idadi ya timu nne zitakazokwenda kushiriki michuano ya kimataifa mwakani, sambamba na klabu za Yanga, Simba na Azam FC ambazo zimemalizika kwenye nafasi tatu za juu.

Katika timu hizo nne Simba na Yanga zitakwenda kucheza Ligi ya Mabingwa Afrika, huku Azam FC na Biashara zitashiriki michuano ya Kombe la Shirikisho.

Hii itakuwa mara ya kwanza kwa Biashara United kushiriki michuano ya kimataifa toka ilipopanda daraja misimu miwili iliyopita.

error: Content is protected !!