July 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

‘Bia chupa 2-4 kwa siku basi’

Dk. Stephen Kebwe, aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro

Spread the love

SERIKALI imesema, unywaji pombe kupindukia unasababisha watoto wengi kuzaliwa katika hali isiyo ya kawaida kiafya na kiakili. Anaandika Dany Tibason … (endelea).

Mbali na hilo serikali imesema, unywaji mzuri wa pombe ni kati ya bia chupa mbili hadi nne ndani ya saa 24 kwa wanaume na bia mbili hadi tatu kwa akina mama ndani ya saa 24.

Pia kiwango hicho hakiwezi kusababisha madhara kwa afya ya mwanadamu na iwapo mtu atakunwa bia kuzidi hapo, atakuwa amepitiliza hivyo kuwa katika hatari ya kupata madhara.

Kauli hiyo imetolewa leo bungeni na Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Stephen Kebwe alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalum, Fatuma Mikidadi (CCM).

Mbunge huyo alitaka kujua ni kiwango gani cha unywaji wa pombe ambacho hakiwezi kumsababishia madhara mnywaji.

Awali katika swali la msingi la Mbunge wa Viti Maalum, Kidawa Saalehe (CCM) alitaka ni madhara gani ya vileo vikali, sigara bangi na mirungi kwa mtoto aliyetumboni mwa mama?

Dk. Kebwe amesema, yapo madhara mengi ambayo huweza kumpata mtoto ambaye yupo tumboni kwa mama yake pindi mama atapotumia vilevi hivyo.

Amesema, baadhi ya madhara ni kupungua ukuaji wa ubongo kwa mtoto aliyepo tumboni mwa mama anayetumia vilevi vikali.

Matatizo mengine ni mtoto kuzaliwa akiwa na athari zinazotokana na pombe na dawa za kulevya ambazo huathiri mfumo wa uzazi ikiwa ni pamoja na kuzaa mtoto mwenye utindio wa ubongo.

Amesema, matatizo mengine ni pamoja na kuharibika kwa mimba hususan ambazo hazijafikisha umri wa miezi mitatu sambamba na kuzaa watoto njiti.

error: Content is protected !!