August 17, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Benzema afikisha mabao 50 UEFA

Karim Benzema

Spread the love

BAADA ya jana kupachika mabao mawili katika mchezo uliowakutanisha timu yake ya Real Madrid dhidi ya Borussia Dortmund uliomalizika kwa sare ya mabao 2-2 katika dimba la Santiago Bernabeu, hatimaye Karim Benzema amefikisha jumla ya mabao 50 katika michezo aliyocheza ya klabu bingwa barani ulaya.

Benzema ambaye jana alipachika mabao hayo mawili katika dakika ya 28 na 53 alijiunga na klabu hiyo tangu mwaka 2009 akitokea klabu ya Olympic Lyon inayoshiliki ligi kuu nchini Ufaransa amecheza michuano hiyo kwa misimu saba akiwa na Real Madrid na kufikisha idadi hiyo ya mabao.

Licha ya kufunga idadi hiyo ya mabao, Benzema anaingia katika rekodi ya wachezaji waliofunga mabao mengi katika ligi hiyo sambamba mfaransa mwenzake ambaye ni nyota wa zamani wa Arsenal na Barcelona Thierry Henry kwa kufunga mabao 50.

Wachezaji pekee wanaoshikilia rekodi ya kufunga mabao zaidi ya 50 katika historia ya michuano hiyo ya klabu bingwa barani ulaya toka kuanzishwa kwake ni Cristiano Ronaldo, Lionel Messi, Raul na Ruud van Nistelrooy katika nyakati tofauti za uchezaji wao.

Michuano hiyo ambayo jana ilifikia tamati katika hatua ya makundi na kufanya jumla ya timu 16 kuvuka katika hatua ijayo ya mtoano ambapo ratiba hiyo itapangwa kesho baada ya kumalizika kwa michezo ya leo ya kombe la Europa.

error: Content is protected !!