Saturday , 20 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Benki yamwaga neema shule 5 Dar
Habari Mchanganyiko

Benki yamwaga neema shule 5 Dar

Spread the love

BENKI ya NMB imekabidhi msaada wa vifaa mbalimbali vyenye thamani ya Sh.39 milioni kwa shule tano za Temeke jijini Dar es Salaam huku ikisisitiza dhamira yake ya kuendelea kusaidia mipango ya maendeleo ya sekta ya elimu nchini kote. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Vifaa vilivyokabidhiwa ni pamoja na mabati 600, madawati 100 na meza 50 yatakayonufaisha Shule ya Msingi Chem Chem, Shule ya Msingi Azimio, Shule ya Msingi Mtoni, Shule ya Msingi Magurumbasi na Shule ya Sekondari Kibasila.

Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Donatus Richard (katikati), akimkabidhi Katibu Tawala Mkoa wa Dar es Salaam, Hassan Rugwa, sehemu ya msaada wa madawati 100 kwa ajili ya Shule ya Msingi, Chemchem ya Mbagala, pia NMB imekabidhi mabati 600 kwa shule tatu za msingi, pamoja na viti 50 na meza 50 kwa ajili ya Shule ya Sekondari Kibasila, zilizopo wilayani Temeke. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam jana.

Akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano hayo iliyofanyika Sekondari ya Kibasila, Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Donatus Richard alisema jitihada za benki hiyo zinalenga kuunga mkono jitihada za Serikali za kuboresha maendeleo ya sekta ya elimu.

“Serikali imefanya kazi kubwa ya kuweka miundombinu ya sekta ya elimu. Shule nyingi mpya zimejengwa na Serikali ya awamu ya sita. Kama benki, tunaona ni muhimu kuunga mkono juhudi za kuinua sekta hii ndomaana tumejikita kutoa vifaa vya shule nchi nzima,” alisema

Aliongeza, “Kama benki, tunatoa asilimia moja ya faida yetu kila mwaka kusaidia sekta ambazo tuimezipa kipaumbele katika mkakati wetu wa Uwajibikaji kwa Jamii (CSR) ambao unalenga sekta kama vile afya, elimu na dharura. Kama sehemu ya mpango wetu wa CSR, leo tunakabidhi bidhaa zenye thamani ya 39m/- na tunaamini hii itasaidia kuboresha mazingira ya kujifunzia katika shule zitakazonufaika,”

Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Donatus Richard (wa tatu kulia), akimkabidhi Katibu Tawala Mkoa wa Dar es Salaam, Hassan Rugwa, sehemu ya msaada mabati 600 kwa ajili ya shule tatu za msingi zilizopo wilaya ya Temeke, pia NMB imekabidhi madawati 100 kwa shule moja ya msingi, pamoja na viti 50 na meza 50 kwa ajili ya Shule ya Sekondari Kibasila. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam jana.

Awali, Mbunge wa Temeke, Dorothy Kilave alisema msaada huo umekuja wakati muafaka hasa wakati huu ambapo wilaye yake imeeanza kutekeleza kampeni yake ya ‘Boresha vya Kale’ ambayo pamoja na mambo mengine inalenga kukarabati shule kongwe wilayani humo.

“Serikali imeanza kujenga shule mpya kote nchini ila siai mama wilaya, tumeona  ni wakati muafaka wa kuboresha shule kongwe ili zisibaki nyuma zikiwa katika hali mbaya ndiyo maana tukaja na kampeni hii. Tunaishukuru Benki ya NMB kwa kuunga mkono juhudi zetu na tunaamini msaada wao utafanikisha kampeni yetu.” Kilave alisema.

Kwa upande wake Katibu Tawala wa Wilaya ya Temeke Hassan Rugwa aliipongeza benki hiyo kwa kuendelea kuunga mkono wilaya hiyo na kuongeza kuwa benki hiyo imekuwa mstari wa mbele na bidhaa nyingi zinalenga watu wa ngazi ya chini.

“Kuna kambuni nying katika sekta ya kibenki na fedha lakini Benki ya NMB ni ya kipekee. Hivi karibuni, benki ilitangaza bidhaa yake ya mkopo wa elimu ambayo itanufaisha watoto kutoka familia masikini. Napenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru NMB kwa kuendelea kutuunga mkono,” alisema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wauguzi, madaktari 1000 kugawiwa mitungi ya Oryx Gas

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gas na Taasisi ya Doris Mollel Foundation...

Habari Mchanganyiko

Tanzania yachaguliwa Makamu wa Rais Tume ya Shirika la Hali ya Hewa Duniani

Spread the love  TANZANIA kupitia Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)...

Habari Mchanganyiko

NEMC yaonya wanaojenga bila tathmini ya mazingira

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC),...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

error: Content is protected !!