January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Benki ya walimu yaanza kuuza hisa

Gratiani Mukoba, Rais wa CWT

Spread the love

KASSIM Majaliwa-Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), amevitaka vyama vya wafanyakazi nchini kuiga mfano wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) wa kuanzisha mradi ambao utaleta manufaa kwa wanachama wake. Anaandika Sarafina Lidwino … (endelea).

Majaliwa ametoa wito huo leo wakati wa uzinduzi wa uuzwaji wa hisa za Benki tarajiwa ya Walimu, ambao umefanyika jijini Dar es Salaam.

Akimwakilisha Waziri Mkuu Mizengo Pinda kwenye uzinduzi huo, Majaliwa amesema, Serikali inaunga mkono kuanzishwa kwa benki hiyo ambayo ina lengo nzuri la kuwainua walimu na wananchi kwa ujumla.

“Niwapongeze wadau wote walioshiriki katika mafanikio ya benki hii, pamoja na Mwenyekiti mwazilishi wa banki hii, Gratian Mukoba, kwa kupigania na kuvumilia kashifa zote na hatimaye leo mmefanikisha,”amesema.

Baada ya kuzindua uuzwaji wa hisa hizo zinazoanzia Sh.500, Majaliwa naye alinunua hisa za Sh. 1.5 milioni kutoka kwa Mwalimu Commecial Bank (MCB).

Naye Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba, amewapongeza CWT kwa kufanya shughuli hiyo kwa uwazi na kwa kufuata maadili na nidhamu zote.

Amesema, kwa niaba ya serikali na wizara ya fedha, wameunga mkono asilimia 100 kuanzishwa kwa mradi huo, kwani utaisaidia serikali katika kupambana na umaskini nchini.

“Tuwatakie kila la kheri katika umoja wenu, msiachane, muendele kuongeza matawi kwenye mikoa mingine ili kuongeza wanunuzi wa hisa kwenye benki yenu. Pia niwatake walimu wote nchini warudi kwenye nyumba yao maana tayari imeishakamilika,”amesesema Nchemba.

Aidha, Rais wa CWT, Gratiani Mukoba amesema, benki hiyo ipo kwa ajili ya watu wote, na kwamba sio walimu pekee.

“Kuna takribani waalimu laki mbili nchini, hivyo wote wakijitokeza kununa hisa itasaidia kuwakomboa kiuchumi na kuongeza kipato serikalini kwa njia ya makato ya kodi,”amesema Mukoba.

error: Content is protected !!