Friday , 19 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Benki ya NMB yagawa vifaa tiba Arusha
Habari Mchanganyiko

Benki ya NMB yagawa vifaa tiba Arusha

Spread the love

SEKTA ya afya ni sekta muhimu kwa maendeleo ya jamii na kwa kulitambua hilio, Benki ya NMB imeshirikiana na Serikali kupitia Wizara ya Afya kuboresha huduma za Afya kwa Wilaya ya Arusha kwa kutoa msaada wa vifaa tiba vyenye jumla ya thamani ya zaidi ya Sh. milioni 26 katika kituo vya Afya – Mkonoo. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Vifaa tiba hivyo vilivyotolewa ni  vitanda 10 vya kujifungulia kwa kina mama pamoja na vitanda 10 vya kulaza wagonjwa wa kawaida.

Aidha, katika Kituo cha Afya Levolosi waliwakabidhi mabenchi 20 ya kusubiri huduma na kukalia kwa wasindikizaji.

Kabla ya kukabidhi vifaa hivyo, Afisa Mkuu wa Huduma Shirikishi wa NMB, Nenyuata Mejooli alisema vifaa hivyo ni moja ya ushiriki wa benki hiyo katika maendeleo ya jamii.

Alisema na NMB ni benki inayoongoza Tanzania hivyo wanao wajibu wa kuhakikisha jamii inayowazunguka inafaidika kutokana na faida wanayoipata.

Alisema Benki ya NMB imekuwa ikipokea maombi mengi ya kuchangia katika miradi ya jamii, lakini benki imejikita zaidi katika maeneo ya elimu, afya na misaada muhimu katika nyakati ngumu kama za majanga.

“Tumekuwa mstari wa mbele kuchangia huduma za kijamii kwa lengo la kurejesha sehemu ya faida yetu kwa jamii.

“Kwa zaidi ya miaka 10 mfululizo, Benki ya NMB  imekuwa ikitenga asilimia moja  ya faida yake kama sehemu ya uwajibikaji kwa jamii inayoizunguka,” alisema

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

Habari Mchanganyiko

Carbon First, Ruangwa wasaini makubaliano ya biashara ya hewa ukaa

Spread the love  KAMPUNI ya Carbon First Tanzania Limited na Halmashauri ya...

Habari Mchanganyiko

CBE yawakumbuka wenye mahitaji maalum Jangwani

Spread the loveCHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimetoa msaada mbalimbali na...

Habari Mchanganyiko

Mume auwa mke kwa kumchoma visu, ajisalimisha Polisi

Spread the loveJACKSON Kalamji (49), anashikiliwa na Jeshi la Polisi jijini Mwanza,...

error: Content is protected !!