Saturday , 20 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Benki ya NBC yaweka kambi Kanda ya Kaskazini, kuamsha sekta ya utalii, biashara na kilimo
Habari Mchanganyiko

Benki ya NBC yaweka kambi Kanda ya Kaskazini, kuamsha sekta ya utalii, biashara na kilimo

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongella akizungumza na wageni waalikwa wakati wa hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na benki ya NBC
Spread the love

BENKI ya Taifa ya Biashara (NBC) imeelezea dhamira yake ya kukuza na kuchochea ukuaji wa kiuchumi katika mikoa ya Kanda ya Kaskazini kwa kukuunga mkono jitihada zinazofanywa na serikali katika kukuza sekta ya Utalii, kilimo, ufugaji na Biashara. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Mkuu wa Wilaya ya Babati, Lazaro Twange akizungumza na wageni waalikwa wakati wa hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na benki ya NBC kwa ajili ya wateja wadogo na wakubwa wa mkoani Manyara ili kujadili fursa za biashara, kutambulisha huduma mpya za benki hiyo kupitia huduma yake ya NBC Biashara Club.

Katika kuthibitisha dhamira yake hiyo, viongozi waandamizi wa benki hiyo wakiwemo wawakilishi wa bodi ya wakurugenzi, wakurugenzi na wakuu wa Idara mbalimbali wa benki hiyo mwishoni mwa wiki walitembelea mikoa ya Manyara, Arusha na Karatu wakilenga kukutana na wateja wao katika sekta hizo ili kwa pamoja waweze kujadili fursa za kibiashara, mipango ya ukuaji na huduma mpya zitolewazo na benki hiyo.

Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Dk Kassim Hussein akizungumza na wageni waalikwa wakati wa hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na benki hiyokwa ajili ya wateja wadogo na wakubwa wa Mkoani Manyara hivi karibuni ili kujadili fursa za biashara, kutambulisha huduma mpya za benki hiyo kupitia huduma yake ya NBC Biashara Club.

Akizungumza kuhusu matukio hayo, Mkurugenzi wa Kitengo cha Biashara kwa wateja binafsi Benki ya NBC, Elibariki Masuke alisema kupitia hatua hiyo wameweza kukutana na wateja wao na hiyo hatua kupata wasaa wa kutambulisha huduma zao mpya sambamba na kupokea mrejesho kuhusu mahitaji ya wateja wao hususani kipindi hiki ambacho mikoa hiyo ipo kwenye mkakati wa kuboresha zaidi sekta ya utalii.

“Rais wetu na serikali kwa ujumla wamefanya jitihada kubwa katika kuinua sekta ya utalii na hivyo sisi kama wadau muhimu kwenye hilo tumeona tuje kumuunga mkono kufanikisha adhma yake hiyo. Kupitia huduma yetu ya NBC Biashara Club tumeweza kukutana na walengwa ambao ni wateja wetu na tumeweza kujadili na kuwasilisha huduma zetu mpya zinazoendana na dhamira hii kuu ya kukuza utalii ikiwemo huduma yetu ya mikopo ya magari ya utalii huku dhamana ikiwa ni magari yenyewe,’’ alisema.

Mkurugenzi wa Kitengo cha Biashara kwa wateja binafsi Benki ya NBC, Elibariki Masuke (kushoto) akibadilishana mawazo na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongella wakati wa hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na benki hiyo mwishoni mwa wiki kwa ajili ya wateja wadogo na wakubwa wa jijini Arusha ili kujadili fursa za biashara, kutambulisha huduma mpya za benki hiyo kupitia huduma yake ya NBC Biashara Club.

Alitaja huduma nyingine kuwa ni pamoja na huduma ya mikopo ya zana za kilimo yakiwemo matrekta huku dhamana ikiwa ni kifaa chenyewe, mikopo ya wazabuni pamoja na mikopo ya wafanyabiashara wanaonza biashara inayofahamika kama ‘NBC Kua Nasi’.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kitengo cha Biashara kwa wateja wadogo na wa kati wa benki hiyo, Bw Elvis Ndunguru alisema kupitia dhamira hiyo, benki hiyo inatarajia kuboresha zaidi huduma yake ya malipo ya POS ili kuongeza ufanisi katika ukusanyaji wa mapato yakiwemo yale ya fedha za kigeni.

“Sekta ya utalii inachangia zaidi ya asilimia 25 ya fedha za kigeni. Kwa hiyo uboreshaji wa mfumo wa ukusanyaji wa mapato ni muhimu sana hivyo mwisho mwa mwezi huu tunataraji kuzindua huduma yetu ya POS iliypboreshwa zaidi kwa ajili ya malipo ya Dolan a Shilingi. Na pia tunatarajia kuongeza huduma ya American Express kwenye mfumo huo ili kuhudumia pia wateja wa Marekani,’’ alisema.

Akizungumzia hatua ya benki hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Bw John Mongella alisema imekuja wakati muafaka kwa kuwa kupitia jitihada za Rais Samia Suluhu na serikali za kuboresha sekta ya utalii nchini, ukanda huo unatarajia kupokea watalii wengi zaidi mwaka huu, hivyo maboresho zaidi katika huduma za kifedha ni muhimu.

Meneja Bidhaa na Huduma za Kibenki kutoka Benki ya NBC, Jonathan Bitababaje akizungumza na wageni waalikwa wakati wa hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na benki ya NBC kwa ajili ya wateja wadogo na wakubwa wa mkoani Manyara ili kujadili fursa za biashara, kutambulisha huduma mpya za benki hiyo kupitia huduma yake ya NBC Biashara Club.

“Kwa mfano mkoa wetu wa Arusha tunategemea utalii kwa asilimia 80.Tayari Rais ameshafanya jitihada nyingi za kufanikisha ukuaji wa sekta ya utalii kilichobaki ni sisi viongozi na wadau wengine kumuunga mkono kama wanavyofanya NBC kwasasa. Tunaamini jitihada zao hizi mbali na sekta ya utalii tutaona mabadiliko makubwa katika sekta za kilimo, biashara na ufugaji pia…tunawashukuru sana,’’ alisema.

Akiishukuru benki hiyo kwa niaba ya wateja wote, Muhandisi Matoleo Ouden ambaye ni mfanyabiashara jijini Arusha alisema kupitia ujio wa viongozi hao waandamizi wameweza kupata wasaa wa kuwasirisha mahitaji yao kwa viongozi waandamizi wa benki hiyo ili yaweze kufanyiwa kazi na maamuzi kutoka ngazi ya juu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Gardner Habash wa Clouds Fm afariki dunia

Spread the loveALIYEKUWA mtangazaji wa kipindi cha Jahazi kinachorushwa na kituo cha...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wauguzi, madaktari 1000 kugawiwa mitungi ya Oryx Gas

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gas na Taasisi ya Doris Mollel Foundation...

Habari Mchanganyiko

Tanzania yachaguliwa Makamu wa Rais Tume ya Shirika la Hali ya Hewa Duniani

Spread the love  TANZANIA kupitia Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)...

Habari Mchanganyiko

NEMC yaonya wanaojenga bila tathmini ya mazingira

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC),...

error: Content is protected !!