Thursday , 18 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Benki Ya NBC Yashiriki Uzinduzi Kongamano La Kigoda Cha Mwalimu Nyerere
Habari Mchanganyiko

Benki Ya NBC Yashiriki Uzinduzi Kongamano La Kigoda Cha Mwalimu Nyerere

Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Rais Mstaafu Jakaya Kikwete (kushoto ) akisalimiana na Madaraka Nyerere ambae ni mtoto wa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alipowasili Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa ajili ya uzinduzi wa Kongamano la 13 la Kigoda cha Mwalimu Nyerere uliofanyika leo chuoni hapo.
Spread the love

BENKI ya Taifa ya Biashara (NBC) imeshiriki kwenye uzinduzi wa Kongamano la 13 la Kigoda Cha Mwalimu Nyerere uliofanyika leo tarehe 8 Juni, 2022 katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM). Kongamano hilo la siku tatu limezinduliwa na Mkuu wa Chuo hicho, Rais Mstaafu wa Awamu ya Jakaya Kikwete, ambaye aliongoza viongozi mbalimbali wa kisiasa, kitaaluma na kiserikali akiwemo Waziri Mkuu mstaafu Mizengo Pinda. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Rais Mstaafu Jakaya Kikwete (wa pili kushoto ) akiwaongoza viongozi mbalimbali wa kisiasa, kitaaluma na kiserikali wakati wa maandamano mafupi kueleka ukumbuni kwa ajili ya uzinduzi wa Kongamano la 13 la Kigoda cha Mwalimu Nyerere uliofanyika leo chuoni hapo. Wengine ni pamoja na Waziri Mkuu mstaafu Mizengo Pinda (wa pili kulia), Mwenyekiti wa Kigoda cha Mwalimu, Profesa Rwekaza Mukandala,(wa tatu kulia), Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa William Anangisye (Kushoto) na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Profesa Florens Luoga (Kulia).

Mbali na kuwa mmoja wa wadhamini muhimu katika kongamano hilo, Benki ya NBC kupitia tawi lake la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam iliandaa banda maalum kwa ajili ya kutoa huduma zake kwa washiriki wa kongamano hilo sambamba na kushiriki katika kongamano hilo.

Maofisa wa Benki ya NBC tawi la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akiwemo Meneja Maendeleo Biashara tawi hilo, Fredrick Massawe (Kulia) na Ofisa Mauzo wa tawi hilo, Amir Mhina wakiwahudumia baadhi ya wateja ambao ni wanafunzi wa Chuo hicho, Anna Kipuzi na Maria Kipuzi waliotembelea banda la maonesho ya huduma za benki hiyo lilipo nje ya ukumbi wa Kongamano la 13 la Kigoda cha Mwalimu Nyerere chuoni hapo.

“Benki ya NBC tunatambua mchango na falsafa za Hayati Mwalimu Julius Nyerere si tu kitaifa bali pia katika uanzishwaji wa benki hii. Hii imekuwa ni moja ya sababu muhimu kabisa ya sisi kuendelea kuwa mstari wa mbele katika kufanikisha na kushiriki katika masuala yote yanayohusiana na Hayati Mwalimu Julius Nyerere likiwemo Kongamano hili muhimu,’’ alisema Anne Mwaisaka, Meneja wa Benki ya NBC Tawi la chuo hicho.

Maofisa wa Benki ya NBC tawi la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akiwemo Meneja Maendeleo Biashara tawi hilo, Fredrick Massawe (Kulia) na Ofisa Mauzo wa tawi hilo, Amir Mhina wakiwahudumia baadhi ya wateja ambao ni wanafunzi wa Chuo hicho waliotembelea banda la maonesho ya huduma za benki hiyo lilipo nje ya ukumbi wa Kongamano la 13 la Kigoda cha Mwalimu Nyerere chuoni hapo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Carbon First, Ruangwa wasaini makubaliano ya biashara ya hewa ukaa

Spread the love  KAMPUNI ya Carbon First Tanzania Limited na Halmashauri ya...

Habari Mchanganyiko

CBE yawakumbuka wenye mahitaji maalum Jangwani

Spread the loveCHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimetoa msaada mbalimbali na...

Habari Mchanganyiko

Mume auwa mke kwa kumchoma visu, ajisalimisha Polisi

Spread the loveJACKSON Kalamji (49), anashikiliwa na Jeshi la Polisi jijini Mwanza,...

Habari Mchanganyiko

Serikali yatoa ajira watumishi 46,000, yatangaza utaratibu mpya kuajiri

Spread the loveSERIKALI imetangaza nafasi za ajira za watumishi wa umma 46,000...

error: Content is protected !!