Wednesday , 24 April 2024
Home Kitengo Michezo Benki ya NBC yakabidhi kombe la ubingwa wa ligi kuu kwa Yanga
MichezoTangulizi

Benki ya NBC yakabidhi kombe la ubingwa wa ligi kuu kwa Yanga

Spread the love

MDHAMINI Mkuu wa ligi ya NBC, Benki ya Taifa ya Biashara(NBC) leo Ijumaa aimekabidhi kombe la ubingwa wa ligi kuu ya soka Tanzania bara kwa timu ya Yanga ambayo ndiyo bingwa kwa msimu wa 2022/2023. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Hafla ya kukabidhi kombe la ubingwa imefanyika katika uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya, huku ikishuhudiwa na mamia ya wapenda soko wakazi wa jiji hilo na meneo ya jirani.


Akikabidhi kombe hilo kwa Yanga mkuu nwa mkoa wa Mbeya, Juma Homera aliishukuru benki ya NBC kuwa mdhamini mkuu wa ligi kuu ya Tanzania bara na kusema kuwa udhamini wa NBC umekuwa na matokeo chanya kwa soka la Tanzania.

“Udhamini wa NBC umewezesha kuongeza ushindani kwenye ligi na kuboresha soka letu. Leo hii tunajivunia kuwa na ligi bora barani Afrika tukishikilia nafasi ya tano. Naipongeza sana benki ya NBC kwa kufanya mambo makubwa katika ligi na soka la nchi yetu kwa ujumla,” alisema Homera.


Mkuu huyo wa mkoa aliipongeza timu ya Yanga kwa kutwaa ubingwa na kusema kuwa haikuwa rahisi kwa timu hiyo kuibuka kinara wa ligi kutokana na ushindani mkali kutoka kwa timu pinzani.

Kwa upande wake mkurugenzi wa fedha wa NBC, Barnabas Waziri alisema NBC itaendelea kuwa mdhamini mkuu wa ligi na kuongeza kuwa benki hiyo  pia itaendelea kutoa mchango katika sekta ya michezo kwa upana wake.

“Pamoja na soka, tumekuwa tukisaidia michezo mingine kama riadha kupitia NBC Dodoma marathon. Nia yetu ya kusaidia sekta ya michezo hapa nchini ni thabiti na tutaendelea kusaidia,” alieleza

Mkurugenzi huyo alisema udhamini wa NBC kwenye ligi kuu umekuja na maboresho kadhaa ikiwa ni pamoja na kutoa bima kwa wachezaji wa ligi kuu pamoja na familia zao pamoja na mikopo ya mabasi kwa vilabu vinavyoshiriki ligi.

“Juzi tumezindua kombe jipya lenye hadhi na ambalo leo litakabidhiwa kwa bingwa wa ligi. Ili kuongeza hamasa kwa wachezaji na makocha, tumekua tukitoa tuzo mbalimbali kwa makocha na wachezaji bora wa mwezi,” alisema.

Mkurugenzi huyo aliipongeza Timu ya Yanga kwa kutwaa ubingwa kwa msimu wa pili mfululizo na pia alizipongeza timu zote zilizoshiriki ligi ambayo ushindane wake umekuwa ni mkubwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Michezo

Arsenal dhidi ya Chelsea ngoma nzito leo EPL

Spread the love  Leo kutakua na mchezo mkali sana pale kwenye ligi...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

Habari za SiasaTangulizi

Shibuda amlima waraka mzito Bulembo

Spread the loveMKONGWE wa siasa nchini, John Shibuda amemshukia kada maarufu wa...

error: Content is protected !!